Na Mahmoud Zubeiry, DAR ES SALAAM
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF)
limesimamisha mchakato wa uchaguzi wa klabu
ya Simba SC hadi hapo klabu hiyo itakapounda
Kamati ya Maadili ambayo itasikiliza masuala ya
kimaadili kuelekea uchaguzi huo.
Akizungumza na Waandishi wa Habari makao
makuu ya TFF, katikati ya Jiji la Dar es Salaam
mchana wa leo, rais wa TFF, Jamal Emil Malinzi
amesema kwamba Simba SC inatakiwa kuwa
imekwishaunda Kamati ya Maadili hadi kufika
Juni 30, mwaka huu.
Malinzi amesema kwamba hatua hiyo imefuatia
TFF kupokea malalamiko mengi juu ya ukiukwaji
wa maadili kwa baadhi ya wagombea na
wanachama wa klabu hiyo.
Malinzi amesema kwamba baada ya kuundwa
kwa Kamati hiyo Maadili itasikiliza malalamiko
yote ya kimaadili yanayougubika mchakato wa
udhaguzi huo, ambao awali ulipangwa kufanyika
Juni 29, mwaka huu.
Malinzi amesema kwamba kwa sasa Kamati ya
Utendaji ya Simba SC iliyopo madarakani chini
ya Mwenyeiiti wake, Alhaj Ismail Aden Rage
itaendelea kuiongoza klabu hiyo hadi hapo
mchakato wa uchaguzi utakapokamilika.
Sunday, 15 June 2014
MALINZI ASIMAMISHA UCHAGUZI SIMBA SC
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment