Yamekwisha: Wachezaji wa Cameroon walitarajiwa kuondoka usiku wa jana kwenda Brazil
KIKOSI cha Cameroon kilitarajiwa kuondoka jana usiku mjini Younde kuelekea Brazil baada ya kutatuliwa kwa mgogoro wa posho zao.
Waziri
Adoum Garoua alisema jana “Kila mmoja yuko tayari kuondoka Saa 3:30
(usiku wa jana) kwenda Brazil. Kila kitu kimefafanuliwa. Hakuna matatizo
zaidi,”.Wachezaji
wa Simba Wasiofinguka jana waligoma kupanda ndege kwenda Brazil kwa
ajili ya Kombe la Dunia ili kushinikiza malipo ya posho za kushiriki
michuano hiyo na kubaki
katika hoteli yao mjini Yaounde, wakati Waandishi wa Habari walikuwa
nje ya ofisi za Shirikisho la Soka Cameroon kupata maelezo juu ya sakata
hilo.
Ndege
ilitarajiwa kuondoka Yaounde Saa 3:00 asubuhi ya jana kwenda Brazil,
wakati Cameroon inacheza mechi yake ya ufunguzi Ijumaa na Mexico.
No comments:
Post a Comment