Mambo safi: Luke Shaw akiwa ameshika jezi ya Man United baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 31.5
BEKI
wa kimataifa wa England, Luke Shaw amekamilisha uhamisho wa Pauni
Milioni 31.5 kutua Manchester United kwa mkataba wa miaka minne kupiga
kazi Old Trafford.
Mchezaji
huyo amekamilisha vizuri vipimo afya katika Uwanja wa mazoezi wa
United, Carrington na ameambiwa atakuwa beki wa kushoto chaguo la kwanza
la kocha Louis van Gaal.
Inafahamika
amehakikishiwa mamba na beki mkongwe mwenye umri wa miaka 33, Patrice
Evra, ambaye atabakia United, anatarajiwa kupunguziwa majukumu klabuni
hapo.
No comments:
Post a Comment