Sunday, 15 June 2014

RAGE: TUMEPATA FEDHA ZA KUJENGA UWANJA, NATAKA KUWEKA REKODI SIMBA, NAACHA MILIONI 300 ZA USAJILI, KABLA SIJAONDOKA NAJENGA GHOROFA MOJA YA HOSTELI BUNJU

UCHAGUZI ni habari kubwa
kwasasa katika klabu ya
Simba, lakini kuna maisha
mengine yanaendelea ikiwemo
utekelezaji wa mpango wa
kujenga uwanja wa kisasa
katika eneo la Bunju, jijini Dar
es salaam.
Mtandao huu jana iliripoti
kuwa uongozi wa Simba sc
umepelekea magereda na
malori ambayo kwa kutwa
nzima yalikuwa yanafanya kazi
ya kuondoa udongo mweusi
uliopo eneo hilo na kuweka
udongo mpya utakaofaa
kuotesha nyasi za uwanja.
Jitihada za kuwatafuta
viongozi wa Simba zilifanywa
ili kupata ufafanuzi juu ya
suala hilo na mtandao huu
umejitahidi kumtafuta rais wa
Simba anayemaliza muda
wake, Ismail Aden Rage ili
kutoa ufafanuzi wa zoezi hilo
na pesa zimepatikana wapi
wakati huu Simba ikitarajia
kufanya uchaguzi juni 29
mwaka huu.
Kuna watu walihusianisha
mpango huo na kampeni
kuelekea uchaguzi. Kuna
wagombea fulani (majina
tunayo) walikuwa
wanahusishwa na kutoa fedha
hizo ili kujisafishia njia, lakini
halikuwa jibu sahihi na ikabidi
Rage asakwe ili atoe maelezo.
Katika mahojiano yake na
mtandao huu, Rage amesema
sasa wameshaanza mambo
baada ya kupata fedha mahali
fulani (hakutaka kutaja) na
suala la wanachama kwenda
na majembe, mapanga
wameacha.
“Uko katika hatua nzuri kuna
kitu ambacho wataalamu wa
udongo wanaita, wametoa ule
udongo mweusi, wameanza
kuweka udongo ambao utafaa
kupandia nyasi za uwanja”.
Alisema Rage.
‘Na kama unakumbuka mara
ya kwanza tulipoanza
kukarabati au kuujenga,
tuliwaomba wanachama,
wakaenda na mapanga na
majembe.”
“Sasa tumeacha, kwasababu
tulipata pesa mahali fulani,
sasa kuna magereda na malori
yanafanya kazi ya kutoa huo
mchanga ambao haufai na
kuweka mchanga unaofaa kwa
kuotesha nyasi”. Aliongeza
Rage.
Rais huyo aliyekuwa na
mvutano mkali na wanachama
wa Simba pamoja na viongozi
wenzake wakati wa uongozi
wake alisema ndani ya siku
chache zijazo watawakaribisha
waandishi wa habari ili
wakapige picha, waone uwanja
ulivyokuwa mzuri,
ulivyopendaze na hatua nzuri
ambazo wanazo.
Hata hivyo, Rage alisema
wamechoshwa na kutumia
gharama kubwa za kuweka
kambi Hotelini, hivyo anataka
kujenga Hosteli za wachezaji
kabla hajakabidhi madaraka
kwa uongozi mpya.
“Lakini ninafanya vilevile
mpango, kwasababu tunatumia
gharama nyingi sana
kuwaweka wachezaji wetu
Hotelini wakati tunapofanya
kambi”.
“kwasababu eneo hilo ni zuri,
tunataka ikiwezekana kabla
sijaondoka, angalau nipate
michoro au niweze kuweka
msingi au ghorofa moja
ikibidi, tujenge hosteli katika
muda huu mfupi uliobaki”.
Alisema Rage.
Kuhusu usajili, Rage alisema
anataka kuweka rekodi
ambayo haijawahi kutokea
Simba ambapo atawaachia
viongozi wajao kitita kirefu
cha pesa, si chini ya milioni
300 kwa ajili ya usajili.
“Sasa hiyo nawaachia viongozi
wajao ambao ninakusudia
kuweka rekodi ambayo
haijatokea Simba tangu miaka
yote, kwa maana ya kwamba
nitakapoondoka mimi
nitawaachia pesa za wao
kufanya usajili si chini ya
milioni 300 watazikuta pale
klabu”.
“Sivyo kama mimi nilipoingia
sikukuta hata shilingi moja
nilikuta madeni basi, hiyo
ndiyo nataka niweke tofauti
yangu mimi ambaye
ninaithamini klabu yangu hii”.
Alieleza Rage.
Nako upande wa pili,
mwenyekiti wa klabu hiyo,
Yusuf Manji ameongezewa
muda wa mwaka mmoja na
wanachama wa Yanga ili
kukamilisha baadhi ya ahadi
zake ikiwemo ujenzi wa uwanja
wa kisasa maeneo ya
Jangwani.
Hatua za Simba zinaweza
kumshitua na akaongeza kasi.
Simba na Yanga ni klabu
kongwe ambazo hazina hata
uwanja wa mazoezi.
Azam fc ni klabu pekee yenye
uwanja wake wenye ubora wa
kimataifa uliopo Mbande,
chamazi, nje kidogo ya jiji la
Dar es salaam.
Mbeya City fc ambao
wameshiriki kwa mara ya
kwanza ligi kuu msimu
uliopita, wana mpango wa
kujenga uwanja wao maeneo
ya Iwambi jijini Mbeya.

No comments:

Post a Comment