![Kocha wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameibuka na kudai kuwa kutokuwa na huruma kwake ndiko kulikomfanya akaipatia mafanikio United.](http://taarifa.co.tz/wp-content/uploads/2014/06/fergie.jpg)
Kocha
wa zamani wa Manchester United Sir Alex Ferguson ameibuka na kudai kuwa
kutokuwa na huruma kwake ndiko kulikomfanya akaipatia mafanikio United.
Raia huyo wa Uskochi alikuwa na sifa kubwa kwenye safari yake ya ukocha United, ila amefichua namna alivyokuwa mkali na asiyekuwa na huruma na kuweza kushinda fikra zote, jambo ambalo lilimsaidia kupata mafanikio aliyoyapata.
“Nililipwa ili niendelee kushinda, hiyo ndio ilikuwa kazi yangu, hivyo nilikuwa sina huruma.” Siwezi kulikataa hilo. Ferguson aliwaambia wajumbe kwenye tuzo za EY World Enterpreneur jana.
Huna budi kuwa na mtu mwenye nguvu wakati unapowaongoza watu. Na nina nguvu nzuri sana”.
Hata wakati mambo yalipoenda kinyume na yeye, Ferguson alikubali kuwa uhakika binafsi ilikuwa ni sifa muhimuya uongozi.
“Sikuwahi kujitilia mashaka mwenyewe”, aliongeza.
“Hata wakati wa kipindi kigumu, kwa mara ya kwanza nilipojiunga Manchester United, nilijua kuwa nilichokuwa nakifanya kilikuwa sahihi”
No comments:
Post a Comment