NYOTA
wa Ufaransa, Frank Ribery bado yupo kwenye hatihati ya kucheza Fainali
za Kombe la Dunia katokana na kutokuwa fiti kiasi cha kutosha, ingawa
kwa vyovyote Samir Nasri hawezi kuchukuliwa kuziba pengo lake hata
akienguliwa kikosini.
Kiungo
huyo wa Bayern Munich alitajwa katika kikosi cha mwisho cha wachezaji
23 wa Ufaransa kwa ajili ya Kombe la Dunia Brazil juzi, lakini hakuna
matumaini kama atapona haraka.
Remy
Cabella wa Montpellier - ambaye wakati fulani aliwahi kutakiwa na
Newcastle - na Alexandre Lacazette wa Lyon wamewekwa mkao wa kula kwa
ajili ya mmoja wao kuchukua nafasi ya Ribery iwapo hatapona ndani ya
muda unaotakiwa.
No comments:
Post a Comment