Sunday, 15 June 2014

BENZEMA APIGA MBILI UFARANSA IKIUA 3-0 KOMBE LA DUNIA

SHERIA ya teknolojia langoni hatimaye leo
imetumika kikamilifu kumaliza utata wa bao
Ufaransa ikiitandika mabao 3-0 Honduras katika
mchezo wa Kundi E Kombe la Dunia. Karim
Benzema amefunga mabao mawili mjini Porto
Alegre dakika za 45 kwa penalti na 72, wakati
bao lingine Noel Valladares alijifunga dakika ya
48 na kulazimika sheria ya teknolojia kwenye
mstari wa goli kutumika ili kuhakikisha kama
lilikuwa bao halali.
Wilson Palacios wa Honduras alionyeshwa kadi
ya pili ya njano na kuwa nyekundu baada ya
kumsukuma Paul Pogba kwenye boksi na
Benzema akafungwa kwa penalti.
Kikosi cha Ufaransa kilikuwa; Lloris, Debuchy,
Varane, Sakho, Evra, Pogba/Sissoko dk57,
Cabaye/Mavuba dk65, Matuidi, Valbuena/Giroud
dk78, Benzema na Griezmann.
Honduras: Valladares, Beckeles, Bernardez/
Osman Chavez dk46, Figueroa, Izaguirre, Najar/
Claros dk58, Wilson Palacios, Garrido, Espinoza,
Bengtson/Boniek Garcia dk46 na Costly.

No comments:

Post a Comment