Wednesday, 18 June 2014

MARADONA ACHAMBUA KOMBE LA DUNIA, ASEMA "MULLER HANA MISULI, PEPE 'BWEGE BWEGE' NA HISPANIA BADO INA NAFASI, RONALDO ABADILISHE UCHEZAJI"

SHUJAA wa Argentina na Kombe la Dunia, Diego Maradona anafikiri mshambuliaji wa Ujerumani, Thomas Muller 'hana misuli' lakini alijitahidi kuisambaratisha Ureno na akamponda Pepe alipewa kadi nyekundu ya 'kibwege'.
Pepe alipewa kadi nyekundu baada ya kumvaa Muller akiwa chini na kuanza kumpa mikwara uso kwa iso akiwa kama anampiga kichwa, jambo ambalo lilimfanya refa Milorad Mazic kumtoa nje, na kumsaidia mshambuliaji huyo wa Ujerumani kuongoza katika mbio za ufungaji bora.
Hiyo ilitosha kwa Ujerumani kuwa na mwanzo mzuri na Ureno kuanza vibaya na Maradona anajaribu kuelezea tathmini yake katika mechi za mwaka huu.

Mshindi wa Kombe la Dunia: Diego Maradona aliiongoza Argentina kushinda Kombe la Dunia mwaka 1986 na ana yake ya kusema juu ya michuano ya 2014 'Unprofessional': Pepe made referee Milorad Mazic's decision easy after shoving his head into Muller
'Ubwege': Pepe alimfanya refa Milorad Mazic aamue kwa urahisi kumpa kadi nyekundu baada ya kumpelekea kichwa Muller

AMESEMAJE KUHUSU CRISTIANO RONALDO?

Diego Maradona anafikiri Cristiano Ronaldo aliangushwa na kucheza kibinafsi, akashindwa kuipasua ngome ya Ujerumani.
"Cristiano Ronaldo asingeruhusiwa kucheza kama ambavyo anacheza Real Madrid,"amesema Maradona.
"Aliwekewa ulinzi mkali asipite na alitakiwa kujaribu kufumua mashuti ya mbali.
"Mara ya mwisho alifunga bao kwenye Kombe la Dunia dhidi ya Korea Kaskazini mwaka 2010. 
"Anatakiwa kuisaidia timu yake kwenye mechi mbili zilizosalia dhidi ya Marekani na Ghana iweze kuingia 16 Bora.'
Alipoulizwa kuhusu kiwango cha Muller dhidi ya Ureno, Maradona aliliambia gazeti la Time la India kwamba; "Hana misuli, lakini amewasambaratisha,".
Mshindi huyo wa Kombe la Dunia mwaka 1986 pia alimkadia Pepe kwa nidhamu mbovu iliyoigharimu timu yake.
"Ilikuwa ni ajabu wan a kumuona akifanya upumbavu wa hivyo,"alisema Maradona. 
"Ni kweli Muller aliigiza kama ameumizwa na kujiangusha, lakini hakukuwa na haha ya Pepe kufanya alichokifanya. 
"Ubwege wake uliiumiza Ureno na kupoteza matumaini kabisa ya kuzinduka katika muda uliokuwa umesalia kwenye mchezo huo,".
Ujerumani ilikuwa tayari inaongoza kwa mabao 2-0 wakati Pepe anatolewa nje.
Lakini Maradona alikuwa ana maoni pia juu ya maamuzi katika mchezo huo, akisema: "Ile penalti iliyowapa bao la kuongoza Ujerumani ilikuwa laini sana.
Opinionated: Maradona was in charge of Argentina at the 2010 World Cup and had his say on this year's tournament
Maoni yake: Maradona alikuwa kocha wa Argentina katika Fainali za Kombe la Dunia mwaka 2010 na michuano ya mwaka huu anatoa maoni yake

"Joao Pereira alimchezea rafu Mario Gotze, lakini kiungo huyo wa Bayern Munich aliongeza chumvi na refa wa Serbia akaamini. Lakini si kitu kwa Ujerumani, walikuwa bora kama wakati wote,".
Haikuwa Ureno pekee waliokuwa na wiki mbaya, Hispania pia walipihgwa mabao 5-1 na Uholanzi.
Lakini Maradona anasema kikosi cha Vicente del Bosque 'hakijafa'. "Hispania inaweza kuzinduka kupitia kwa wachezaji wake wakongwe,"amesema. 
"Del Bosque afikirie upya mipango yake na kuwapa nafasi wachezaji kama Koke kucheza mechi zote muhimu Uwanja wa Maracana. Ni kufa na kupona kwa timu hiyo ambayo imeshinda mataji matatu tangu 2008,". 
"Pamoja na hayo, wanaweza kufufua matumaini ya kusonga mbele kama wataifunga Australia mabao mengi na Chile ikafungwa mabao mengi na Uholanzi,".
Chelsea vs Manchester United: Fernando Torres (left) and Robin van Persie battle for the ball
Chelsea vs Manchester United: Fernando Torres (kushoto) na Robin van Persie wakigombea mpira

No comments:

Post a Comment