KIUNGO Ander Herrera amekamilisha uhamisho
wa Pauni Milioni 29 kwenda Manchester United
akitokea Athletic Bilbao.
Klabu hiyo ya La Liga ilikataa ofa ya timu hiyo
ya kocha Louis van Gaal, lakini baada ya
mchezaji huyo kufuzu vipimo vya afya Carrington
jana, dili hilo limekamilishwa.
Nyota huyo mwenye umri wa miaka 24 sasa
anakuwa mchezaji wa kwanza kabisa kusajiliwa
na Man United chini ya kocha mpya, van Gaal
aliyerithi mikoba ya David Moyes Old Trafford.
No comments:
Post a Comment