ILIMCHUKU
sekunde 52 Cristiano Ronaldo kuithibitishia dunia kwama amepona na yuko
fiti kwa Fainali za Kombe la Dunia wakati Ureno ikiitandika Jamhuri ya
Irelando mabao 5-1 jana katika mchezo wa kirsfiki Uwanja wa MetLife.
Akiwa
hajacheza mechi tangu baada ya Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya mwezi
uliopita, Ronaldo aliwatoka mabeki wa Ireland baada ya kugusa mpira kwa
mara ya kwaza na kufumua shuti lililolenga lango. Ulikuwa ujumbe tosha
CR7 amerejea.
Mbele
ya Roy Keane, mchezaji mwenzake wa zamani wa Manchester United,
aligongesha mwamba, alitoa pasi, na mara mbili akakaribia kufunga na
hakika alionyesha kabisa yuko tayari kwa kipute cha Brazil. Mabao ya
Ureno yalifungwa na Hugo Almeida dakika za tatu na 37, Richard Keogh
alijifunga dakika ya 19 na Vierinha dakika ya 77 na Fabio Coentrao na
bao pekee la Ireland lilifungwa na McClean dakika ya 52.
Amerudi:
Ronaldo alicheza vizuri na kuonyesha kwamba amepona na yuko tayari kwa
ajili ya mechi ufunguzi dhidi ya Ujerumani wiki ijayo![Raring to go: Cristiano Ronaldo was in the thick of the action as Portugal beat Ireland in their warm-up game](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/06/11/article-2654655-1EA5F92C00000578-622_634x410.jpg)
![Raring to go: Cristiano Ronaldo was in the thick of the action as Portugal beat Ireland in their warm-up game](http://i.dailymail.co.uk/i/pix/2014/06/11/article-2654655-1EA5F92C00000578-622_634x410.jpg)
Shuti: Cristiano Ronaldo akifumua shut jana
No comments:
Post a Comment