Monday, 23 June 2014

KIPRE TCHETCHE ‘ALIVYOTUA YANGA LEO’...


MSHAMBULIAJI Kipre Herman Tchetche leo amezima uzushi kwamba yuko kwenye mpango wa kuhamia Yanga SC, baada ya kuibukia kwenye mazoezi ya timu yake, Azam FC.
Nyota huyo kutoka Ivory Coast aliwasili jana Dar es Salaam kutoka kwao Abidjan alipokwenda kwa mapumziko baada ya msimu na asubuhi ya leo akaibuka mazoezini Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.
Kipre alilakiwa na kocha Mcameroon Joseph Marius Omog na kuzungumza naye kwa dakika kadhaa kabla ya kujiunga na wenzake kwa mazoezi.
Kipre Tchetche akikabidhiwa tuzo yake na Jemadari Said

No comments:

Post a Comment