Thursday, 5 June 2014

PIGO UHOLANZI, VAN PERSIE AUMIA, SASA DAKTARI KUAMUA HATIMA YAKE KOMBE LA DUNIA

MSHAMBULIAJI wa Uholanzi, Robin Van Persie sasa atatakiwa kumuona daktari baada ya kuumia nyonga akiichezea timu yake hiyo jana katika ushindi wa 2-0 dhidi ya Wales mjini Amsterdam.
Wazi kocha Louis Van Gaal atakuwa anaumia sana kichwa kwa maumivu ya mshambuliaji huyo wa Manchester United, zikiwa zimebaki siku zisizozidi 10 kabla ya kucheza na Hispania katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Dunia.
Kabla ya kuumia na kutoka, Van Persie alitengeneza bao la kwanza lililofungwa na Arjen Robben wakati bao la pili lilifungwa na Jeremain Lens.

Maumivu: Mshambuliaji wa Uholanzi, Robin van Persie akitoka nje baada ya kuumia nyonga jana
Assist: Van Persie's first-half shot was parried into the path of Arjen Robben who opened the scoring
Mpishi: Lakini kabla ya kutoka, Van Persie alisababisha bao la kwanza lililofungwa na Arjen Robben

No comments:

Post a Comment