MWANZO
mzuri kwa Neymar akifunga mabao mawili usiku huu, wenyeji Brazil
wakianza vyema Fainali za Kombe ka Dunia kwa ushindi wa 3-1 dhidi ya
Croatia Uwanja wa Corinthias, mjini Sao Paulo.
Croatia waliotawala sehemu ya kiungo, waliuanza vizuri mchezo na kufanikiwa kupata bao la kuongoza dakika ya 11.
Sifa
zimuendee Olic aliyepiga krosi nzuri kwa Nikica Jelavic na katika
harakati za kuokoa, Marcelo wa Brazil aliutumbukiza mpira kwenye lango
lake.
Croatia waliendelea kutawala mchezo baada ya bao hilo, lakini Brazil waiendelea nao kupambana kusaka bao la kusawazisha. Juhudi hizo zilizaa matunda dakika ya 29 baada ya Neymar kuisawazishia Brazil kufuatia shambulizi la kushitukiza- baada ya kipa Julio Cesar kuokoa mpira wa kichwa wa Jelavic na kuanzisha shambulizi haraka. Brazil ilipata bao la ushindi kwa penalti dakika ya 71 baada ya Fred kujiangusha wakati anakabiliana na Dejan Lovren kwenye eneo la hatari na Neymar akaenda kufunga tena. Oscar alihitimisha ushindi wa Brazil kwa bao la tatu dakika ya 90 na ushei na kuwapa faraja mashabiki wa nyumbani. Kikosi cha Brazil kilikuwa: Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Marcelo, Paulinho/Hernanes dk63, Gustavo, Hulk/Bernard dk68, Oscar, Neymar/Ramires dk88 na Fred. Croatia: Pletikosa, Srna, Corluka, Lovren, Vrsaljko, Modric, Rakitic, Perisic, Kovacic/Brozovic dk61, Olic na Jelavic/Rebic dk78.

No comments:
Post a Comment