Wapenzi wa muda mrefu Richard Laslett na Collin Gunther ambao wamedumu
kwenye mahusiano kwa muda wa miaka 37 wamepata nafasi ya kuwa moja kati
ya wapenzi wa jinsia moja 115 waliofungishwa ndoa kwa wakati mmoja mjini
Toronto, Canada.
Ndoa hizo zimefungwa kwa pamoja na kuwakutanisha wapenzi wa jinsia
moja kutoka maeneo mbalimbali duniani kusherekea nguvu ya mapenzi yao.
Meya wa Toronto Norm Kelly amesema wanandoa hao wamekutana na kufurahia hatua hiyo muhimu ya kufunga pingu za maisha.
Takribani nchi 15 duniani sasa zimeruhusu mapenzi ya jinsia moja .
No comments:
Post a Comment