KOCHA
wa Chelsea, Jose Mourinho anafikiri no vyema Chama cha Soka England
(FA) kikatumia fedha inazokuanya kwa kuwatoza faini wachezaji, klabu na
makocha nchini humo kwa kuchangia miradi ya hisani.
Kuliko
kwenda kuangalia Kombe la Dunia nchini, Mourinho amezuru nchini Ivory
Coast kuwatembelea watoto wenye njaa na waathirika wa ukimwi kama Balozi
wa Umoja wa Mataifa wa Shirika la Chakula.
Mreno
huyo amesema kwamba anataka soka ifanye makubwa zaidi kusaidia mambo
kama ambavyo WFP wanafanya, na akapendekeza FA ichangie faini
inazokusanya kwenye mambo mazuri.
Mei
mwaka huu, Mourinho alipigwa faini ya Pauni 10,000 na FA kwa kutoa
maelezo yaliyowakera wakubwa kwenye vyombo vya habari dhidi ya marefa
baada ya Chelsea kufungwa 2-1 na Sunderland, kipigo ambacho kilifanya
rekodi yake ya kucheza mechi 77 bila kufungwa nyumbani izimwe.
No comments:
Post a Comment