Nenda
nje: Kostas Katsouranis wa Ugiriki (katikati) akitolewa nje kwa kadi
nyekundu, baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano dhidi ya Japan usiku
wa kuamkia leo
SARE
ya bila kufungana kati ya Japan na Ugiriki usikua wa kuamkia leo
imeongeza matumaini ya Ivory Coast kuingia 16 Bora ya Kombe la Dunia
kutoka Kundi C.
Kwa safe
hiyo, Ivory Coast inabaki nafasi ya kwa pointi zake tatu nyuma ya
Colombia yenye poinri sita, wakati Japan na Ugiriki kila moja ina pointi
moja.
Ivory
Coast itamaliza na Ugiriki, wakati Japan itamaliza na Colombia, ambayo
tayari imefuzu. Maana yake Ivory Coast lazima iwafunge Ugiriki kwa
sababu Colombia hawatahitaji kutumia nguvu nyingi tena mbele ya Japan
katika mchezo wa mwisho, zaidi kuwekeza katika mchezo wa kwanza wa
mtoano.
No comments:
Post a Comment