Nyumba hii ipo huko Las Vegas na ina acre 40 na indoor car parking kubwa sana kuingiza magari zaidi ya kumi kwa wakati mmoja. Upande wa mwingine ina zoo humohumo ndani,jet inayopark kwenye airport yako binafsi hapo mjengoni haina haja ya kwenda kwenye public airport. Ukitaka kumiliki hii nyumba inabidi zikutoke $ 48 millioni.
Saturday, 30 November 2013
MBWANA SAMATA NA THOMAS ULIMWENGU KUVAA MEDALI ZA DHAHABU LEO?
AZAM YAMPA MKATABA WA MIAKA MIWILI KOCHA WA AKINA ETO’O
KLABU ya Azam leo imemtambulisha kocha wake mpya, Joseph Marius Omograia wa Cameroon iliyempa Mkataba wa miaka miwili kuanzia leo. Omog anatua Azam akitokea klabu ya A.C Leopards ya Kongo Brazavville ambayo aliiwezesha kutwaa ubingwa wa ligi ya nchi hiyo kwa misimu miwili mfululizo (2012 na 2013) na kumaliza ukame wa mataji wa miaka 30.
![]() |
Mwenyekiti wa Azam FC, Sheikh Said Mohammad kulia akimtambulisha kocha mpya, Omog katikati leo |
MAPENZI NI NOUMA,,KIJANA AUKATA UUME WAKE KUEPUSHA USUMBUFU WA WANAWAKE HUKO TABORA.
Ayubu Mnazi Alphonce(24) ni kijana ambaye amelazwa katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Tabora Kitete akipatiwa matibabu baada ya kuamua kuukata uume wake kwa kutumia wembe mpya ili kuepukana na usumbufu anaoupata kutoka kwa wanawake ambao amekuwa nao kimapenzi........ Imeelezwa kuwa baada ya kutokea mfarakano baina yake na mwanamke mmoja ambaye jina lake halijafahamika,Ayoub aliamua kuingia ndani na kuukata uume wake kwa kutumia wembe mkali na kisha kuutupa nje
Taarifa kutoka Jeshi la Polisi zinaeleza kuwa baba mzazi wa Ayubu baada ya kubaini kuwa mtoto wake alikuwa amejifungia chumbani kwa muda mrefu, aliamua kumgongea mlango na alipopata fursa ya kuingia ndani ndipo alipogundua ukweli juu ya jambo hilo na hivyo kumpeleka Ayubu Kituo kikubwa cha Polisi Tabora ambapo jalada la kesi ya kujidhuru lilifunguliwa.
Hata hivyo hali ya Ayubu kwasasa inaendelea vizuri licha ya kuwa amejikata na kubakisha kipande cha sentimeta 5 huku akisubiriwa kufikishwa mahakamani kwa kutenda kosa hilo la kujidhuru mwenyewe pasipo sababu za msingi.
Tuesday, 12 November 2013
P-FUNK 'MAJANI' APATA AJALI MBAYA AKIWA CHOONI....APASUKA KICHWANI NA KUSHONWA NYUZI 12
HUU NDIO MJENGO MWINGINE WA DIAMOND AMBAO UPO KWENYE HATUA ZA MWISHO ILI KUKAMILIKA
Kijana anayefanya vizuri kwenye muziki wa Bongo Fleva Diamond Platnumz mambo si mabaya kwake baada ya kuonyesha mjengo wake mwingine wa hatari ambao bado upo katika ujenzi.
Kupitia mtandao wa kijamii wa Instagram,Diamond jana ame-share picha ya nyumba hiyo na chini akatia neno..Shuka nayo.
HII ALAMA YA VIDOLE 4 IMEMFANYA MCHEZAJI WA MISRI KUADHIBIWA.
Unaambiwa club ya Al Ahly imemuadhibu mchezaji wake aitwae Ahmed Abdul Zaher kwa kitendo alichofanya cha kuonyesha alama za vidole kama unavyomuona hapo chini ikiwa ni ishara ambayo imekua ikitumiwa na wanaomuunga mkono rais Mohammed Morsi aliepinduliwa July 2013 na kwa sasa anakabiliwa na kesi ya kuchochea mauaji.
PICHA ZA DIAMOND AKIWA NIGERIA KUFANYA VIDEO YA NUMBER ONE REMIX NA MTU MZIMA DAVIDO
![]() |
Anaitwa Mama Hilda,muigizaji mkongwe nchini Nigeria |
niwasili nchini hapa,lengo likiwa ni moja tu,
kuunganisha music wetu na wenzetu wa Nigeria,nitashoot video
ya number one remix
with my nicca Davido ,pamoja na kumalizia kazi niliyofanya
na mwanamziki mwingine wa hapa
Nigeria..kikubwa ni kuendeea kuwapa
mashabiki zangu kile haswa mnachokistahili kutokana na
sapoti kubwa
mnayoendelea kunipa..
JANGA JINGINE NCHINI UFILIPINO,WATU ZAIDI YA 10,000 WANAHOFIWA KUFARIKI.
PICHA ZA MASTAAWANAPOJUTIA KUWA NA TATTOO MAMBO KAMA HAYA HUTOKEA
Producer Pharrell Williams alishawahi kukiri kuwa alipata maumivu makali sana wakati anafuta tatto alizochora wakati wa ujana wake na akajutia kitendo hicho. Alikuwa muoga wa magonjwa atakayopata baada ya tattoo kufutwa na mionzi mikali kwenye mwili wake inayoweza kusababisha saratani na magonjwa mengine.
Saturday, 9 November 2013
MANCHESTER UNITED V ARSENAL.OLD TRAFFORD KESHO,HIZI NDIZO TAKWIMU ZA TIMU HIZI
Tayari Mechi 10 zimeshachezwa kwenye Ligi na Arsenal bado wanachanja mbuga wakiwa Tayari Mechi 10 zimeshachezwa kwenye Ligi na Arsenal bado wanachanja mbuga wakiwa hawajafungwa tangu wabamizwe 3-1 na Aston Villa kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi Msimu huu.
MOURINHO ALIA NA RATIBA LIGI KUU ENGLAND
MENEJA wa Chelsea Jose Mourinho amedai Watu ambao wanatengeneza Ratiba ya Ligi Kuu England wanaicheka Timu yake.
Akiongelea kuhusu Mechi yao ya Ligi ya
Jumamosi na West Bromwich Albion, Mourinho amelalamika kuwa kupewa Siku 3
toka Mechi yao ya UEFA CHAMPIONZ LIGI na Schalke waliyocheza Jumatano
na kucheza tena Jumamosi wakati Klabu za Jiji la Manchester, Man United
na Man City, na Arsenal zina Siku 4 toka Mechi zao za Ulaya sio sawa.
KLABU YA SIMBA YAWEKA WAZI USAJILI MPYA
Kocha Msaidizi wa Simba, Jamhuri Kihwelu 'Julio' alisema nafasi hizo ndizo zimeonekana zina mianya.
Julio, ambaye kikosi chake kina wachezaji 26 alisema wanahitaji kujipanga upya na watawasilisha mapendekezo yao kwa uongozi.
Monday, 4 November 2013
MOYES AWATAKA MAREFA KUMLINDA JANUZAJ KAMA MESSI
Mshambuliaji huyo kinda alikuwa alichezewa rafu na beki huyo wa Fulham, United ikishinda 3-1 Uwanja wa Craven Cottage Jumamosi.
Refa Lee Probert na wasaidizi wake hawakuona tukio hilo wakati linatokea, lakini marudio ya picha za video yanaonyesha vizuri.
HII NDIYO NYUMBA YENYE THAMANI YA DOLA MILLION 48,INA UWANJA WA NDEGE HAPO HAPO NYUMBANI
Nyumba hii ipo huko Las Vegas na ina acre 40 na indoor car parking kubwa sana kuingiza magari zaidi ya kumi kwa wakati mmoja. Upande wa mwingine ina zoo humohumo ndani,jet inayopark kwenye airport yako binafsi hapo mjengoni haina haja ya kwenda kwenye public airport. Ukitaka kumiliki hii nyumba inabidi zikutoke $ 48 millioni.
Saturday, 2 November 2013
MASHABIKI SIMBA WATAKA WACHEZAJI WAKONGWE WARUDISHWE
MASHABIKI WA SIMBA
Mashabiki Simba wamepiga kelele na kutala benchi lao la ufundi libadilike na kuwarudisha wachezaji wakongwe.PINDA, MAWAZIRI HATARINI KUNG'OLEWA
DIAMOND AUTIBUA MSAFARA WA RAIS
Friday, 1 November 2013
LEWANDOSKI ATUMA SALAMU KWA ARSENAL! APIGA HETITRIKI, DORTMUND YAIBONDA STUTTGART 6-1!
Robert Lewandowski amepiga Bao 3 wakati Borussia Dortmund ilipotoka nyuma na kuibamizaStuttgart Bao 6-1 na kutua kileleni mwa Bundesliga.
Karim Haggui aliifungia Stuttgart Bao
lao mapema lakini Sokratis Papastathopoulos akasawazisha kwa kichwa na
Marco Reus kufunga Bao la pili kwa Dortmund.
Ndipo zikaja Bao 3 za Lewandowski na Pierre-Emerick Aubameyang kumalizia Bao la 6.
LIGI KUU UINGEREZA NI PATASHIKA JUMAMOSI HII EMIRATES, ARSENAL v LIVERPOOL!
>>WENGER ANAAMINI GIROUD NI KIBOKO KUPITA ‘SAS’, SUAREZ & STURRIDGE!
>>CHELSEA KUFUNGUA JUMAMOSI ST JAMES PARK NA NEWCASTLE!!
>>MABINGWA MAN UNITED NDANI YA CRAVEN COTTAGE NA FULHAM!!
>>MAN CITY: KIPA JOE HART BENCHI…. PANTILIMON NAMBA 1!!
RATIBA
Jumamosi Novemba 2
[Saa za Bongo]
1545 Newcastle v Chelsea
1800 Fulham v Man Utd
1800 Hull v Sunderland
1800 Man City v Norwich
KOBE HUYU ANAVUTIA SIGARA 10 KWA SIKU
Maajabu hayaishi duniani na kila siku yanajitokeza maajabu mapya ambayo hukuwahi kutarajia kuyashuhudia maishani mwako . Nchini Japan kuna kobe ambaye amejiingiza kwenye tabia ya uvutaji wa sigara na mpaka sasa anavuta sigara kumi kwa siku.
YANGA YAENDELEZA WIMBI LA USHINDI, YAICHAPA JKT RUVU 4 - 0.YAPAA MPAKA NAFASI YA KWANZA.
Kikosi cha Young Africans kilichoanza leo dhidi ya JKT Ruvu
Mabingwa
watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Young Africans leo imekamata kiti cha
uongozi baada ya kuendeleza wimbi la ushindi mfululizo kwa kuichapa timu
ya Maafande wa jeshi la Kujenga Taifa nchini JKT Ruvu kutoka mkoani
Pwani kwa mabao 4- 0 mchezo uliofanyika katika dimba la Uwanja wa Taifa
jijini Dar es salaam.
Kikosi
cha mholanzi Ernie Brandts kiliingia uwanjani kwa lengo la kuhakikisha
kinapata pointi 3 muhimu , jambo ambalo vijana wake walilitekeleza na
kuwapa furaha washabiki, wapenzi na wanachama wa klabu ya Yanga
waliokwepo uwanjani kushuhudia mchezo huo.
Mshambuliaji
Mrisho Ngassa aliipatia Young Africans bao la kwanza dakika ya 3 ya
mchezo kwa shuti kali baada ya kuwatoka walinzi wa JKT Ruvu na kumtazama
amekaa vipi mlinda mlango wa JKT Ruvu na kuukwamisha mpira wavuni.
Dakika
ya 12 ya mchezo, Mrisho Ngassa tena aliwainua vitini mashabiki wa timu
ya Young Africans baada ya kumalizia mpira ulipogwa na Saimon Msuva
kabla ya kuwababatiza walinzi wa JKT Ruvu na kumkuta mfungaji ambaye
aliukwamisha mpira wavuni kwa kichwa.
Mpaka dakika 45 za kipindi cha kwanza zinamalizika, JKT Ruvu 0 - 2 Young Africans .
Kipindi
cha pili cha mchezo ulianza kwa kasi na Young Africans kupata bao la
tatu la mchezo dakika ya 47 kupitia kwa Oscar Joshua ambaye alikutana na
mpira uliokolewa walinzi wa JKT na kumkuta mfungaji ambaye alifunga bao
lake la kwanza tangu ajiunge na klabu ya Yanga miaka mitatu iliyopita.
Mabadiliko
yaliyofanya na kocha mholanzi Ernie Brandts kuwaingiza Reliants Lusajo,
Ibrahim Job na Jerson Tegete yaliongeza kasi na uwezo wa kumiliki
mchezo kwani waliweza kucheza vizuri na kulilinda lango lao lisipatwe na
madhara yoyote.
Dakika
ya 89 Jerson Tegete aliipatia Yanga bao la nne la mwisho katika mchezo
huo kufuatia migongeo ya Saimon Msuva na Ngassa kabla ya kumkuta Tegete
akiwa peke yake na kuukwamisha mpira wavuni.
Mpaka dakika 90 za mchezo zinamalizika, JKT Ruvu 0 - 4 Young Africans
Young Africans: 1.Dida, 2.Twite/Job, 3.Oscar, 4.Cannavaro 5.Yondani/Lusajio, 6.Chuji 7.Msuva 8.Domayo, 9.Kavumbagu/Tegete, 10.Ngassa, 11.Kiiza
Subscribe to:
Posts (Atom)