KLABU ya Chelsea ipo kwenye nafasi nzuri ya
kumsaini Sami Khedira baada ya jana usiku
wakala wake kusema hakuna makubaliano
yaliyofikiwa na Arsenal.
Kocha wa Blues, Jose Mourinho amemsajili beki
wa kushoto Filipe Luis kutoka Atletico Madrid
kwa Pauni Milioni 18 na kuhamishia nguvu zake
kwa kiungo wa Ujerumani, Khedira.
Ilikuwa inafahamika Arsenal ilikubali kutoa Pauni
Milioni 20 kwa Real Madrid kumnunua mchezaji
huyo mwenye umri wa miaka 27, lakini walikuwa
wanasuasua kufika kiwango cha mshahara
anaotaka, Pauni 180,000 kwa wiki.
Pamoja na hayo, wakala wa Khedira, Jorg
Neubauer amesema: "Hatupo katika
mazungumzo na Arsenal. Sifikiri wanweza
kukubaliana ada, vinginevyo ningeambiwa,".
Khedira anavutiwa na Mourinho tangu
anafundisha Real na kocha huyo inafahamika pia
anampenda sana mchezaji huyo.
Thursday, 17 July 2014
UMAFIA HADI ULAYA, CHELSEA YAIPINDUA ARSENAL DILI LA KHEDIRA
Wednesday, 16 July 2014
Tuesday, 15 July 2014
SAMATTA NA ULIMWENGU WAWASILI DAR NA KUSEMA; “TUTAPIGANA KWA NGUZU ZOTE KUUA MAMBA
WASHAMBULIAJI
tegemeo wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mbwana Ally
Samatta na Thomas Emmanuel Ulimwengu wamewasili Dar es Salaam asubuhi ya
leo kujiunga na timu hiyo kwa ajili ya mchezo wa kimataifa dhidi ya
Msumbiji ‘Mambas’ mwishoni mwa wiki.
DIEGO COSTA AMUAHIDI MOURINHO MATAJI BAADA YA KUSAINI MKATABA WA MITANO CHELSEA
Ametua darajani: Diego Costa akemamilisha uhamisho wake Chelsea akitokea Atletico Madri
MSHAMBULIAJI Diego Costa amepania kushinda mataji zaidi baada ya kukamilisha usajili wake Chelsea.
Mzaliwa
huyo wa Brazil, aliiwezesha Atletico Madrid kutwaa taji la La Liga
msimu uliopita, na kuifikisha Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya
walipofungwa na Real Madrid.
MABINGWA WA DUNIA UJERUMANI WALIVYOPOKEWA KIFALME LEO NYUMBANI
Subscribe to:
Posts (Atom)





