Tuesday, 22 July 2014

KHAMIS KIIZA ‘DIEGO’ APIGWA CHINI YANGA SC, OKWI KUENDELEA KUWIKA!

KLABU ya Yanga imembwaga
mshambuliaji wake Mganda,
Khamis Kiiza ‘Diego wa
Kampala’ baada ya kusajiliwa
kwa Wabrazil wawili, Andrey
Coutinho na Geilson Santos
Santana `Jaja`.
Baada ya Jaja kusaini
mkataba wa miaka miwili jana
makao makuu ya klabu ya
Yanga, kulikuwa na utata ni
mchezaji gani atapigwa chini
kati ya Kiiza na Emmanuel
Anord Okwi.
Awali ujio wa Jaja ulielezwa
kuwaweka kitimoto Kiiza na
Okwi, huku mmojawapo
akitakiwa kutolewa kafara.
Taarifa za uhakika ambazo
mtandao huu umezipata ni
kwamba kocha Maximo
amependekeza kuachwa kwa
Kiiza kutokana na ripoti
iliyoachwa na Hans Van Der
Pluijm.
Mzigo huo uliofuatwa chini ya
kapeti unasema kuwa Pluijm
katika ripoti yake
aliyowasilisha kwa viongozi
baada ya kumalizika kwa
msimu uliopita, alisema ili
Emmanuel Okwi acheze Yanga
sc, lazima Kiiza aondolewe.
Kwa kuzingatia mapendekezo
hayo, Maximo amefuata
ushauri huo na sasa Kiiza
rasmi anaondoka Jangwani.
Katika hatua nyingine,
imeelezwa na chanzo cha
uhakika kuwa Maximo
amewabana viongozi wa Yanga
akiwataka wajenge uwanja wa
mazoezi wa Kaunda ili
kuepukana na adhaa
anayoipata.
Maximo amewakazia na
amesema hakuna jinsi, lazima
uwanja huo ujengwe muda huu.
Pia amewataka viongozi
kuboresha vyumba vya jengo
la Jangwani ili wachezaji wote
waishe pale.
Taarifa zinasema, Maximo
amesema haiwezekani timu
kukaa saa mbili kwenye foleni
inapoelekea uwanjani na
kurudi kambini.
Kwa mazingira hayo anataka
wachezaji wake wakae makao
makuu ya Yanga, mitaa ya
Twiga na Jangwani, halafu
uwanja wa Kaunda ujengwe.
Mbrazil, Marcio Maximo
anafahamika kwa kuwa na
msimamo mkali katika mambo
yake.

MATS HUMMELS AKARIBIA KUTUA MANCHESTER UNITED!

MATS-HUMMELS
UPO uwezekano mkubwa kwa Sentahafu wa Germany na Klabu ya Borussia Dortmund Mats Hummels kujiunga na Manchester United kabla Wikiendi hii kufika.

STEVEN GERRARD-KUSTAAFU ENGLAND: ROY HODGSON, MAGWIJI WATOA MAONI!

GERRARD-MECHI100
MENEJA wa England Roy Hodgson amewaongoza Magwiji wa Soka wengi huko Uingereza kummiminia sifa aliekuwa Nahodha wa England Steven Gerrard mara baada ya kutangaza kustaafu kuichezea Nchi yake.

Kuhusu miili na viungo vya Binadamu vilivyogundulika July 21 Dar es salaam.


newss 
Taarifa iliyoanza kusambaa usiku wa July 21 ni kuhusu Mabaki ya miili ya watu ambao wanasemekana zaidi ya 100 kukutwa katika msitu mdogo uliopo eneo la Mpiji,kata ya Mbweni, wilaya ya Kinondoni,ikiwa imetelekezwa.

DIEGO COSTA, FABREGAS WAFANYA VITU VYA AJABU MAZOEZINI..JIONEE HAPA

Mchezaji mpya, Diego Costa akijiandaa kupokea mpira wakati wa mazoezi ya Chelsea kujiandaa na msimu nchini Austria
 WACHEZAJI wapya Diego Costa na Cesc Fabregas wameanza kujifua na timu yao mpya, Chelsea inayofundishwa na Mreno Jose Mourinho amabyo imepiga kambi Austria.
Wawili hao walioajiliwa kutoka Atletico Madrid na Barcelona msimu huu, walionekana wenye furaha na moral ya hali ya juu wakati wa mazoezi yao ya kwanza baada ya kufanya vibaya Kombe la Dunia wakiwa na timu yao ya taifa, Hispania.

ED WOODWARD AWAHAKIKISHIA MASHABIKI MAN UNITED WAPYA WAJA!

MAKAMU MWENYEKITI MTENDAJI wa Manchester United, Ed Woodward, amewaambia Mashabiki wa Klabu hiyo kuwa wategemee ujio wa Wachezaji wapya kadhaa na pia kuhama kwa baadhi ya Wachezaji katika Wiki chache zijazo.
LVG-ROONEY-MAZOEZINI-USA 

United imetumia Pauni Milioni 50 kuwanunua Luke Shaw na Ander Herrera na kauli hii ya Woodward inaleta imani kuwa Meneja mpya Louis van Gaal atapata Wachezaji wengine wapya kabla Msimu mpya kuanza.

KUMEKUCHA ZIARA YA REAL MADRID NCHINI TANZANIA..KIINGILIO CHA CHINI NI SH 5000

KUMEKUCHA. Hivyo ndivyo unavyoweza kusema kuhusu ziara ya kikosi cha wachezaji nyota waliowahi kutamba Real Madrid ya Hispania, maarufu kama Real Madird Legends ambao watazuru nchini mwezi ujao. Wachezaji waliotamba kuanzia La Liga, wakacheza ligi nyingine za Ulaya, Kombe la Ulaya, Ligi ya Mabingwa na Kombe la Dunia waliowahi kuchezea Madrid watakuja nchini Agosti 22.
Wanakuja bongo; Roberto Carlos, Ronaldo Lima, Luis Figo na Zinadine Zidane wanatarajiwa kuzuru na kikosi cha magwiji wa Real Madrid nchini mwezi ujao