Ushindani kati ya Diamond na Ali Kiba ambao siku zote mimi nauita ‘ushindani usio rasmi’ huku wengine wakiutafsiri kama ‘beef’ umetengeneza mitazamo tofauti kati ya wadau wa muziki Tanzania.
Tuesday, 5 August 2014
Diamond Vs Ali Kiba : Nay wa Mitego atamani kutembeza kipigo kikali kukomesha
Ushindani kati ya Diamond na Ali Kiba ambao siku zote mimi nauita ‘ushindani usio rasmi’ huku wengine wakiutafsiri kama ‘beef’ umetengeneza mitazamo tofauti kati ya wadau wa muziki Tanzania.
Ukweli kuhusu wimbo wa Linex: Zitto Kabwe ashiriki kukamilisha lyrics 70%, Adam Juma alipwa pesa ambayo hajawahi kulipwa na msanii yoyote, speech yake yaskika wishoni
Wimbo mpya wa Sunday Mjeda a.k.a Linex unaoitwa Wema kwa Ubaya
unaotarajiwa kutoka hivi karibuni pamoja na video yake umetengenezwa na
producers watatu akiwemo More Fire ambae alisimamia uingizwaji wa
vocals, producer Mona Gangstar ambae yeye alishughulikia mixing na
kumaliziwa kwa producer Tuddy Thomas ambae amefanya mastering.
BREAKING NEWS; YANGA SC YAENGULIWA KOMBE LA KAGAME, AZAM WACHUKUA NAFASI KIGALI
BARAZA la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) limeiengua Yanga SC katika michuano ya Kombe la Kagame na nafasi hiyo kupewa Azam FC, zote za Tanzania.
Yanga SC imeenguliwa kwa sababu moja tu kubwa, kushindwa kuthibitisha kupeleka kikosi cha kwanza pamoja na kocha Mkuu, Marcio Maximo kwa mujibu wa kanuni za mashindano.
Monday, 4 August 2014
Picha mpya ya mtoto wa Kanye West na Kim Kardasian yavutia watu mtandaoni.
VAN GAAL AREJESHA FURAHA MAN UNITED, YAWAFUMUA LIVERPOOL 3-1 NA KUBEBA MWALI WA KIMATAIFA MAREKANI
LOUIS
Van Gaal ametwaa taji la kwanza Manchester United baada ya usiku wa
kuamkia leo kuwachapa mahasimu, Liverpool mabao 3-1 Uwanja wa Sun Life
mjini Miami, Marekani na kubeba Kombe la Kimataifa, michuano ya klabu
kujiandaa na msimu mpya.
Saturday, 2 August 2014
NOOIJ APANGUA KIKOSI STARS, NGASSA NA OSCAR JOSHUA WAPIGWA MKEKA, MOURAD NA MCHA WANAANZA LEO DHIDI YA MAMBAS
KOCHA
Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Mart Nooij
amefanya mabadiliko madogo katika kikosi chake kitakachomenyana na
Msumbiji, Mambas jioni ya leo Uwanja wa Zimpeto mjini hapa.
Nooij
aliyewahi kuifundisha Msumbiji, atamuanzisha Khamis Mcha ‘Vialli’
badala ya Mrisho Ngassa na Said Mourad badala ya Oscar Joshua wakati,
wengine wote ni wale walioanza mchezo wa Dar es Salaam.
Mcha aliingia kumpokea Ngassa kipindi cha pili Dar es Salaam na akafunga mabao yote mawili katika sare ya 2-2 moja kwa penalti.
Nooij
ambaye amesema anakiamini kikosi chake kuelekea mechi ya marudiano ya
hatua ya mwisho ya mchujo kuwania kupangwa kwenye makundi ya kuwania
tiketi ya kucheza Fainali za Mataifa ya Afrika (AFCON) mwakani nchini
Morocco, anahitaji ushindi wa ugenini ili kusonga mbele.
![]() |
| Tuko tayari; Kocha Mart Nooij akiwaongoza vijana wake kuingia Uwanja wa Zimopeto jana tayari kwa mazoezi ya mwisho kujiandaa na mchezo wa leo |
Subscribe to:
Posts (Atom)


