Friday, 11 October 2013

RAIS MSTAAFU MHE.MKAPA AZINDUA KAMPENI YA TUSOME TANZANIA (LET US READ TANZANIA CAMPAIGN).

PIX_1_ddeae.jpg
Rais Mstaafu Mhe. Benjamini William Mkapa ambaye pia ni mgeni rasmi akihutubia vijana mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Kampeni ya tusome Tanzania (Let us read Tanzania) aliyoizindua leo katika viwanja vya Makao Makuu ya Maktaba ya Mkoa jijini Dar es Salaam.

BAADA YA KUMUINGIZIA ZAIDI YA MILLIONI 130 NYIMBO YA POMBE YANGU,,MADEE AJA NA NYINGINE TENA;'TEMA MATE TUWACHAPE'


                       NYUMBA YA MADEE
Kila msanii anapotoa single kali kila mmoja anatamani kusikia itakayofata itakuaje? hii inatokea hata kwa Madee ambae ‘Pombe yangu’ ilimpa nguvu ya kutosha kumiliki chati za radio na TV na hata kumpa show za zaidi ya milioni 100.
Time hii naitumia kukualika kusikiliza single yake mpya ya ‘tema mate tuwachape’ ft Richard


WE NI MWANDISHI WA HABARI NA UNGEPENDA KWENDA BRAZIL KURIPOTI KOMBE LA DUNIA - MAOMBI YATAANZA KUPOKELEWA DESEMBA 7



VITAMBULISHO KURIPOTI KOMBE LA DUNIA
Maombi ya vitambulisho kwa waandishi wa habari (Accreditation) wanaotaka kuripoti Fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika mwakani nchini Brazil kwa Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) yataanza kupokelewa kwa mtandao Desemba 7 mwaka huu kupitia akaunti ya FIFA Media Channel.

HATIMAE WAYNE ROONEY AVUNJA UKIMWA JUU YA SIR ALEX FERGUSON, MANCHESTER UNITED

Wakati mashabiki wa Manchester United wakionyhesha kukata tamaa juu ya uwezo wa meneja wao mpya David Moyes baada ya michezo saba ya ligi kuu ya England,nyota wa klabu hiyo Wayne Rooney bado ana imani kocha huyo atafanya vizuri kama akipewa muda wa kutosha.

Rooney amesema hakufurahishwa na majukumu aliyopewa na Ferguson msimu uliopita,amekili sasa kuwa na furaha pale Old Trafford sababu kubwa ni Moyes kumchezesha kwenye nafasi anayoipenda ya ushambuliaji  tofauti na msimu uliopita ambapo alichezeshwa kwenye nafasi ya kiungo.

‘Kila mtu klabuni alikuwa anajua nafasi niliyokuwa naipenda kucheza,sababu ya mimi kukata tamaa ilikuwa ni kulazimishwa kucheza kwenye nafasi ya kiungo,binafsi sikufurahishwa ila ilinilazimu kucheza kwa ajili ya manufaa ya timu,na ilinibidi wakati furani kuwa mbinafsi ili kunusuru maisha yangu'.

Baada ya mwanzo  mzuri sasa nina furaha na nadhani sasa naweza kukaa meza moja na uongozi wa man utd kwa ajili ya kujadili mambo yangu ya baadae

VITU VYA AJABU VYAKAMATWA KWENYE BANDARI YA MOMBASA


112 
Kontena ambalo lilikuwa na vitu vya nyumbani, limekamatwa likiwa na bidhaa nyingi za ajabu kama mafuvu na vitu vingine vya kutisha ambavyo inasemekana huwa vinatumika kwenye ibada za dini za kishetani. Mzigo huo bado unashikiliwa na mamlaka za Kenya na hii hapa audio ya ripoti nzima pamoja na video ya mzigo wenyewe kama ilivyoripotiwa na Citizen TV

KURASA ZA MAGAZETI YA LEO IJUMAA.

.
.
.
.
.
.