Evans Elieza Aveva amefanikiwa
kumshinda mpinzani wake
Andrew Tupa na kuweka rekodi ya
kuwa kiongozi wa kwanza wa
Simba Sports Club wa ngazi ya
juu kuliko zote kutumia jina la
Rais.
Pia mashabiki wa Geofrey Nyange 'Kaburu'
aliyekuwa anagombea makamu wa rais nao
wameanza kushangilia wakionyesha wamepata
matokeo kwamba amewashinda akina Sued
Nkwabi na Jamhuri Kiwhelo 'Julio'.
Aveva amemshinda Tupa kwa
idadi kubwa ya kura katika
uchaguzi uliofanyika leo kwenye
Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa
Polisi Oysterbay jijini Dar es
Salaam.
Mara baada ya Aveva
kutangazwa mshindi, cheleko
kutoka kwa wafuasi wake
zilianza.
Sunday, 29 June 2014
BREAKING NEWS..Huyu ndiye rais wa kwanza wa simba sports club na makamu wake waliochaguliwa hivi punde..
Saturday, 28 June 2014
Wimbo mpya wa Ben Pol waleta mtafaruku kati ya Adam Mchomvu na Fetty
Baada ya kuutambulisha wimbo mpya wa Ben Pol "Upendo" exclusive kupitia
kipindi cha XXL kinachoendeshwa na B12, Fetty na Adam Mchomvu, kumetokea
na ubishani kati ya Adam na Fetty juu ya wimbo huo ambao unamuonekano
tofauti na jinsi alivyozoeleka Ben Pol
Huku Fetty akiusifia na kuona ni wimbo wenye tofauti nzuri ambao una
mahadhi ya bolingo na hata kusema ni fusion zinazotakiwa
SALIM KIKEKE KUTOKA BBC LONDON,,KING MAJUTO,,ELIZABETH MICHAEL(LULU) MILLARD AYO NA WENGINE WENGI WATAMBA KATIKA TUZO ZA WATU WANAOPENDWA...JIONEE JINSI TUZO ZILIVYOTOLEWA.
King
Majuto akifurahi mara baada ya kupokea Tuzo yake mara baada ya
kutangazwa mshindi wa Kipengele cha Msanii Bora anayependwa wa Kiume.
Friday, 27 June 2014
DAALAL: AVEVA NDIYE KIBOKO YA YANGA, MPENI SIMBA SC MLE RAHA
ALIYEKUWA
Mwenyekiti wa Simba, Hassan Daalal, amewataka wanachama wa klabu hiyo
wampe kura Evans Aveva kwa sababu ndio kiboko ya Yanga.
Dalali amewaambia wanachama wa Simba Wilaya ya Kinondoni waliohudhuria katika mkutano wa kampeni uliofanyika jioni hii kwenye ukumbi wa Urafiki Hall, Ubungo.
Alisema kuwa wanachama wakimchagua Aveva basi watafurahi msimu mzima kama mgombea huyo alipokuwa anaongoza kamati ya usajili ya klabu hiyo.
Dalali amewaambia wanachama wa Simba Wilaya ya Kinondoni waliohudhuria katika mkutano wa kampeni uliofanyika jioni hii kwenye ukumbi wa Urafiki Hall, Ubungo.
Alisema kuwa wanachama wakimchagua Aveva basi watafurahi msimu mzima kama mgombea huyo alipokuwa anaongoza kamati ya usajili ya klabu hiyo.
![]() |
| Mzee Daalal amewomba wana Simba wamchague Aveva |
Subscribe to:
Posts (Atom)


