Mwanariadha wa Afrika kusini Oscar Pistorius
amerejea tena mahakamani kuhojiwa zaidi na
kujibu maswali ya mwendesha mashtaka mkuu
Gerrie Nel katika kesi anayoshtumiwa kwa
kumpiga risasi na kumuua mpenzi wake
mwanamitindo Reeva Steenkamp nyumbani
kwake mwezi februari tarehe 14 mwaka uliopita .
Bwana Nel amekuwa akimwandama Pistorius ,
akisema hakuwa mkweli katika toba yake na
alimfokea mpenzi wake Reeva Steenkamp mara
kwa mara .
Siku ya kwanza ya maswali ya mahakama dhidi
yake Nel alianza kwa kuonyesha picha za kutisha
za kichwa kilichochuruzika damu cha Bi
Steenkamp, baada ya kupigwa risasi na Pistorius.
Mwanariadha huyo anadai hakumuua makusudi
bali alidhani ni mtu alievamia nyumba yake.
Ameiambia mahakama kuwa alimpenda sana
mwanadada huyo Reeva .
Kiongozi wa mashataka amemsuta Pistorious
akisema kuwa alikuwa ni mbinafsi sana kwa
mpenzi wake na kuwa kile alichokijali sana
ilikuwa ni sifa zake na hadhi yake katika jamii.
Pistorious alikanusha madai hayo akisema
anajuta kwanini hakuwahi kumwambia Reeva
kuwa anampenda kupitia ujumbe wa simu ya
mkononi.
Pistorius akitoa ushahidi
Mwanariadha huyo alikuwa na wakati mgumu
kuelezea mahakama kwanini Reeva alimlaumu
kwa kumuonea katika moja ya ujumbe wa simu
ya mkononi wa WhatsApp ambao alimwandikia
Oscar''tangu turejee kutoka cape town
umekuwa ukinionea sana .''
Viongozi wa mashtaka wana imani kuwa
alimuuwa kimakusudi ndani ya choo chake baada
ya kuzozana.
Mwanariadha huyo mlemavu mwenye umri wa
miaka 27, ambaye hana miguu yake yote mawili,
huenda akahukumiwa jela maisha iwapo
atapatikana na kosa la kuuwa.
Kinyume ya hali ilivyokuwa Siku ya Jumanne,
alipolia kizimbani alipokuwa akielezea yaliyojiri
nyumbani kwake kabla na baada ya mauwaji
hayo,
leo alionekana mjasirii na mtulivu akimjibu
Kiongozi wa mashataka ya umma bwana Nel.
Mamake Reeva bi June Steenkamp amesema
kuwa japo aliombwa msamaha na Oscar moyo
wake haukumsamehe kwani hadi hapo Oscar
hakukiiri alimua bali alisisitiza kuwa anaomba
msamaha kwa kusababisha kifo chake..
Bi Steenkamp mahakamani
Bi Steenkamp alishangaa iwapo Pistoriuos
alikuwa anaigiza au la kwani amekuwa akilia na
kutapika mahakamani .
Katika tukio lingine Oscar alikataa katakata kuwa
alifyatua risasi katika mkahawa mmoja
alipoulizwa na kiongozi wa Mashtaka bwana Nel.
Pistorious alisema kuwa hakujua bunduki hiyo
ilikuwa na risasi.
Iwapo hatapatikana na hatia ya kukusudia kuua
Reeva ,basi kulingana na sheria za Afrika Kusini,
Pistorious huenda akashtakiwa kwa kosa la kuua
bila ya kukusudia ambayo hukumu yake ni kati ya
miaka 6- 15 jela.
Mbali na shtaka la mauaji, Pistorius anakabiliwa
na shtaka la kufyatua bunduki hadharani na
shtaka lingine la kumiliki risasi kinyume na sheria.
Friday, 11 April 2014
PISTORIUS HALI YAZIDI KUA TETE MAHAKAMANI.
Thursday, 10 April 2014
HALIMA MDEE ASHIKA NAMBA MOJA KWA WANAWAKE JASIRI AFRIKA
Mbunge wa Kawe (Chadema) Halima Mdee na Mkurugenzi wa Jukwaa la Uchumi la Dunia kwa Bara la Afrika(WEF) Elsie Kanza, ni miongoni mwa viongozi wanawake 11 wa kisiasa kutoka barani Afrika waliotunukiwa tuzo ya kuwa viogozi wanawake wa juu wenye nguvu katika siasa.
Mdee ambaye pia ni Waziri kivuli wa Wizara ya Ardhi, nyumba na Maendeleo ya Makazi, aliunganishwa katika orodha ya wanawake jasiri katika masuala ya siasa barani Afrika kwa mwaka 2012.
WADADA WALIOKUWA WANAFANYISHWA BIASHARA YA NGONO CHINA WARUDISHIWA PASSPORT ZAO
sasa kwa mujibu wa chanzo cha habari cha kuaminika ni kwamba Candy na Wenzake wamerudishiwa Passport zao ila simu zao za mkononi wamepokonywa, Candy anawashukuru watanzania wote kwa kuonyesha kuguswa na kwa vyombo vya habari kwa kuweka hewani waraka wao, na sasa hivi wako wanatafuta shughuli za kufanya kwani zipo nyingi sanaaaa China.a
EXCLUSSIVE NDOA YA DIAMOND NA WEMA SEPETU MWEZI WA NANE pita hapa kujua zaidi....
Akizungumza na Amani jijini Dar es Salaam juzikati, Hassan alisema amepiga mahesabu ya kinyota kwa wapenzi hao na kubaini kuwa, Agosti ndoa yao itafungwa mahali popote nchini Tanzania
MAMBO KUMI NILIYOJIFUNZA BAADA YA ROBO FAINALI YA UEFA CHAMPIONS LEAGUE:
Inawezekana kabisa Falcao akawa
amepishana
na bahati kama Owen alivyoenda Madrid
2: Koke anastahiki kuanza timu ya taifa Spain
mbele ya Xavi au Xabi
3: Si vibaya kumuiga alokutangulia kazini, leo
Pep
amekopa maarifa kwa Heyckens walikuwa
wepesi na wenye haraka akiendelea hivi
anaweza kutetea taji.
4: Ukitaka kucheza dhidi ya Messi zungumza na
Simeone anampatia kweli sio kawaida
5: Psg walimkosa aina ya akina (Benitez), Blanc
hajui kucheza knockout
6: Bale bado Madrid haiwezi ama haijafanikiwa
kujengwa kupitia yeye, wanamuhitaji Ronaldo
alie fiti kuvuka panapofuata
7: Mourinho ana mdomo mchafu lakini akili yake
na maamuzi ni ya kitanashati, bonge la kocha
8: Walau ukutane na bayern na sio hawa Atletico
kwa sasa, wana TIMU sio wachezaji, kuwafunga
inabidi upigane kwa aslimia 150
9: Unataka nusu fainali iliyo bora sasa weka
maombi iwe Atletico V/s Bayern na Chelsea V/s
Madrid
10: Diego Simeone V/s Rodgers yupi kocha bora
mwaka huu?????? Hapo mtanisaidia wenyeme ila
SIMEONE HUYU DAAAAHHHH acha nibaki na jibu
langu moyoni nahisi ushalijua
Wednesday, 9 April 2014
SIJUI NI BANGI AU POMBE ZILIZOMSUMBUA DUDU BAYA KUMKATA MAMA YAKE SIKIO NA KUTOKOMEA NALO. SOMA MKASA MZIMA HAPA
Kupitia U Heard ya leo na Gossip Cop, story ni
kuhusu Dudu Baya kumkata skio mama yake
mkubw, kwa madai kuwa anamloga ndio maana
hafanyi vizuri katika kazi zake za mziki.
Kwa mujibu wa mdogo wake kabisa (baada ya
kuzaliwa yeye) amethibitisha kutokea kwa tukio
hilo
"yah kafanya hivyo, ni jambo la
kusikitisha unajua ni hivyo, lakini sasa ndio hivyo
kashafanya, kaenda kule kwa mama mkubwa
kamkata skio, sababu haijulikani ni kwasababu
gani kaenda kufanya hivyo, hata kama alikuwa
na sababu halikuwa jambo la busara kumkata
skio"
"nilienda nikamuuliza nani amemkata skio
akasema ni mheshimiwa, akadai kwamba alikuwa
anamwambia anamloga sijui nini, mambo
ambayo hayana hatia ya msingi kwa ujumla,
kwasababu hata ukiangalia yeye ni motto wala
haumwi chochote wala wala mwanae hawaumwi
ni mzima sasa amemroga nini.......

