Tuesday, 8 July 2014

Watu wanane wamejeruhiwa mmoja akiwa hali mahututi kufuatia mlipuko katika mgahawa mjini Arusha

Watu wanane wamejeruhiwa mmoja akiwa hali
mahututi kufuatia mlipuko katika mkahawa mjini
Arusha Tanzania
Mlipuko huo ulitokea Jumatatu jioni na polisi
wangali wanachunguza kilichousababisha.
Kwa mujibu wa shirika la habari la AFP, mlipuko
huo ulitokea Jumatatu jioni na kuwajeruhi watu
wanane huku mmoja akiwa hali mahututi.
Haijulikani kilichosababisha mlipuko huo.
Kufika sasa afisaa mkuu wa shirika la ujasusi
nchini humo anakutana na wandishi wa habari.
Taarifa zaidi punde tutakapozipata.

TETESI ZA SOKA ULAYA..HAWA NDIO WACHEZAJI WANAOTARAJIWA KUAMIA TIMU HIZI..

Salim Kikeke's photo.

Uhamisho wa Luis Suarez kutoka Liverpool kwenda Barcelona bado unasuasua kutokana na kutokubaliana jinsi ya kukamilisha ada ya pauni milioni 75 (Daily Mail), beki wa kulia kutoka Ufaransa Mathieu Debuchy, 28, anatarajiwa kuwa na vipimo vya afya Arsenal, akijiandaa kuhama kutoka Newcastle kwa pauni milioni 7.9 (Guardian), Newcastle huenda wakapewa Joel Campbell, 22, kama sehemu ya makubaliano ya Debuchy kwenda Arsenal (Newcastle Cronicle), Arsenal pia wanaweza kuwapa Newcastle beki wa kulia Carl Jenkinson, 22, katika makubaliano hayo (Daily Mail),

Diamond Platnumz kamzawadia hili gari mama yake leo July 07.

90bdyIngawa hayupo Tanzania lakini hakungoja mpaka arudi ndipo akabidhi zawadi hii badala yake alichokifanya ni mara baada ya kukamilisha kila kitu kinachoihusu gari hii Diamond Platnumz aliwapatia mameneja wake kwa ajili ya kuiwasilisha kwa mama yake.

MBUNGE WA ARUSHA MJINI GODBLESS LEMA ATOA USHIRIKINO KATIKA UANDAAJI WA VIDEO YA DINI YA ALBUM YA KIARANGA CHA KUKU CHINI YA KAMPUNI YA MULTIMEDIA PRODUCTION..JIONEE PICHA AKIWA LOCATION

MBUNGE GODBLESS LEMA AKIJARIBU KUTAZAMA KWA MAKINI WAKATI SHOOTING IKIIENDELEA
LEMA AKIWA PAMOJA NA DIRECTOR WA MULTIMEDIA PRODUCTION  ISAAC CHIWANGA

Wednesday, 2 July 2014

Hichi ndicho alichokiandika adam mchomvu baada ya ugomvi kwenye kipindi cha xxl.

Clouds FM Kimenuka Watangazi wa Kipindi cha XXL Wapigana Live On Air

leo karibu na mwisho wa kipind cha xxl
watangazaj wa kipind hiko wamegombana
live kwenye kipind mpaka ray alipokuja na
kuwazimia mics!
kisa ni compilation album ya fiesta.
Nini maoni yako kuhusu mwenendo wao na
nani alikuwa Source au influencer wa
ugomvi?
Audio ya Ugomvi huo Coming Soon

Tuesday, 1 July 2014

HANS POPPE: F.O.S. NI UKUTA WA CHUMA, SIMBA SC SASA WAPINZANI WATAISIKIA KWENYE BOMBA


MWENYEKITI wa Friends Of Simba (F.O.S.), Zacharia Hans Poppe amesema umoja wao ni sawa na ukuta wa chuma, maana yake wapinzani wa Simba SC katika soka ya Tanzania sasa wasitarajie mteremko kwa klabu hiyo.
Kwa miaka mitatu sasa Simba SC haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara na pia haijashiriki michuano ya Afrika.
Lakini baada ya kigogo wa F.O.S., Evans Elieza Aveva kuchaguliwa kuwa Rais wa kwanza wa klabu hiyo Jumapili, Simba SC inatarajiwa kurejesha makali yake.
Mwenyekiti wa F.O.S., Zacharia Hans Poppe amesema Simba SC sasa itacheza mpira

Kapteni wa zamani wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), Poppe amesema kwamba Friends Of Simba ni ukuta wa chuma.