Katika yale yaliyosikika mfululizo kuhusu staa wa soka DUNIANI, Cristiano Ronaldo kuna
ishu ya kuachana na mpenzi wake, ipo ya sanamu kubwa kujengwa nyumbani
kwao Ureno kama ishara ya kuheshimu anavyoipa sifa nzuri nchi hiyo
duniani, lakini pia ana tuzo yake ya Ballon d’Or, mwanasoka bora wa
kiume duniani.
Ubora
wake unampa thamani kubwa, wakala wake ametangaza dau kubwa kwa klabu
yoyote ambayo itakuwa tayari kumnunua staa huyo muda wowote kuanzia
sasa.


