Mbuzi mmoja katika Kijiji cha Kakanjuni Kenya amezaa mbuzi mwenye vichwa viwili vilivyoungana huku akiwa na midomo miwili, tukio hili limewashangazawengi walioshuhudia huku wengine wakihisi kwamba mbuzi huyo ni mkosi.
Kahaso Ngumbao ambaye
ndio anamfuga mbuzi huyo alitarajia mbuzi huyo angezaa mapacha kama
kawaida yake lakini imekuwa tofauti, Wanakijiji walitaka kumuua kwa
madai kuwa ni mkosi kutokana na mila za jamii hiyo.
Kwa sasa mwenye mbuzi huyo kuamua kumpeleka mbuzi wake Makao makuu ya Kilimo kwa ajili ya kumhifadhi wanakijiji wasimuue.
“Nilikuwa
natafuta njia ya kupatia msaada wa huyu mnyama maana hawezi na
nikiachiwa mimi huenda nikashindwa saa nyingine.. nikiachia watoto
hawawezi kumlea vile ambavyo labda ningekuwa mimi mwenywe” — Kahaso Ngumbao
Afisa wa Kilimo, Wanyama na Samaki aliahidi kuwa Serikali ya kaunti hiyo itatafuta mahali mbadala na kumhifadhi mbuzi huyo.
No comments:
Post a Comment