Mvua hiyo iliyonyesha majira ya saa 4 za usiku ilidumu kwa muda wa masaa mawili ikiambatana na upepo mkali na mawe yaliyopelekea watu hao kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa na kuharibu mazao pamoja na miti .
Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alifika eneo la tukio akiwa sambamba na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya ambao wametoa pole kwa wafiwa pamoja na mikakati ya serikali kuangalia utaratibu wa kusaidia kaya zilizobakia.
Hata hivyo bado idadi kamili ya athari kwa ujumla ukiacha vifo vya watu haijatolewa.
Mi naungana na waombolezaji kuwapa pole ndugu jamaa na marafiki walioondokewa na ndugu zao katika janga hili.
No comments:
Post a Comment