>>VAN PERSIE: MPENI MOYES MUDA!
JIJINI
London, Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, amegeuka mbogo kwa Watu
waliomponda kwa kuwapa Ofu ya Siku 2 Wachezaji wake na huko Manchester,
Nahodha wa zamani wa Arsenal, Robin van Persie, amemtetea Meneja wa
Klabu yake Manchester United, David Moyes, licha ya kukiri walicheza
ovyo Mechi na Olympiacos waliyotwangwa 2-0.
VAN PERSIE: MPENI MOYES MUDA!
Robin van Persie ameieleza Manchester
United kama ni "mbovu" lakini amesisitiza David Moyes anahitaji muda ili
kurekebisha mambo Old Trafford.
Msimu wa Man United ulizidi kudidimia
Jumanne Usiku wakati walipofungwa 2-0 huko Ugiriki na Olympiacos katika
Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ya UCL, UEFA CHAMPIONZ
LIGI.
Ukichukulia Man United, ambao ndio
Mabingwa Watetezi, wapo Pointi 11 nyuma ya Timu ya 4 kwenye Ligi Kuu
England na wapo Pointi 15 nyuma ya Vinara Chelsea, baadhi ya Watu
wamedai Moyes yupo njiani kupigwa Buti.
Lakini Robin van Persie amemtetea Moyes
kwa kusema: “Yeye ni mpya na anahitaji muda. Anafanya bidii pamoja na
sisi. Ni rahisi kumyooshea kidole Meneja lakini ni sisi tunatakiwa
kuleta mafanikio Uwanjani.”
Licha ya kukiri huu ni Msimu mbovu kwao,
Robin van Persie amesisitiza kuwa upo uwezekano mkubwa wa kuwabwaga
Olympiacos katika Mechi ya Marudiano Old Trafford hapo Machi 19.
ARSENE WENGER: AWASHAMBULIA WALIOMPONDA KUWAPA OFU WACHEZAJI!
Arsene Wenger amejibu mapigo kwa kuwashambulia wale waliomponda kuwapa Wachezaji wake Ofu ya Siku mbili.
Akizungumza kabla ya Jumamosi kusafiri
kwenda kucheza na Stoke City kwenye Mechi ya Ligi Kuu England, Wenger
amesema haamini anachosikia.
Amesema: “Tumecheza bila Mapumziko toka
Desemba, hatuna haja ya kumwelezea Mtu kwamba tunahitaji kupumzika!
Sielewi hawa Watu! Tumepumzika Siku mbili!”
Pia Wenger alitoboa kuwa Mesut Ozil
atarejea baada ya kupona tatizo la Paja pamoja na Beki Thomas Vermaelen
ambae huenda akamchezesha kama Fulbeki wa kushoto kwenye Mechi na Stoke.
Ozil, ambae alikosa Penati walipocheza
na Bayern Munich, aliikosa Mechi iliyofuatia ya Ligi na Sunderland
lakini Wenger amesema kukosekana kwake ni kwa sababu ya maumivu.
No comments:
Post a Comment