![Vardy 3](http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2016/02/Vardy-3.png)
Kocha wa Liverpool Jurgen Klopp katika hali isiyokuwa ya kawaida ameibukia na kutoa kauli kuwa nusura ampigie makofi mshambuliaji wa Leicester City Jamie Vardy kutokana na goli alilolifunga dhidi ya Liverpool janausiku.
Jamie Vardy ambaye mpaka sasa ndiyo kinara wa mabao ligi kuu ya England akiwa na jumla ya magoli 18 jana ameisaidia timu yake ya Leicester City kuichakaza Liverpool goli 2-0 katika uwanja wa Anfield.
![Vardy 2](http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2016/02/Vardy-2.jpg)
“Mambo kama haya hutokea hasa unapokuwa kwenye kipindi kizuri kama walivyo Jamie Vardy na Leicester ” alisema Klopp
Kocha huyo wa Liverpool alienda mbali na kusema “Ni msimu mzuri kwa Leicester na Vardy. Walistahili kila pointi waliyoipata kwenye michezo yao na Jamie Vardy amestahili kila goli alilofunga, Ilibaki kidogo tu nimpigie Makofi Jamie Vardy kwa lile Goli alilofunga lakini sikujisikia vizuri kwa ule wakati”.
![Jamie Vardy](http://shaffihdauda.co.tz/wp-content/uploads/2016/02/Jamie-Vardy.jpg)
Kutokana na matokeo ya jana Leicester City inaendelea kuongoza katika msimamo wa Ligi kuu ya England ikiwa na pointi 50 ikifuatiwa na Manchester City wenye pointi 47 Tottenham wamekwea mpaka nafasi ya 3 wakiwa na pointi 45 wakitofautiana na Arsenal walioshuka mpaka nafasi ya 4 kwa tofauti ya magoli.
No comments:
Post a Comment