Saturday, 5 March 2016

Arsene Wenger amchana Thierry Henry


wenfr
Thierry Henry ni mchezaji mwenye heshima kubwa kwenye historia ya Arsenal, baada ya mechi ya Swansea alitoa maoni yake ambayo mashabiki wa Arsenal lazima watampa support.

Henry alisema,“Sijawahi kuona mashabiki wa Arsenal wana hasira kiasi kile baada ya kufungwa na Swansea kwenye uwanja wao nyumbani”. Ukiangalia kwa umakini ni kwamba kweli mashabiki wa Arsenal lazima watakua na hasira kutokana na kupoteza mechi muhimu hasa wakiwa kwenye harakati za kutafuta ubingwa wa EPL.
Wenger akiwa kwenye mkutano na waandishi wa habari aliulizwa swali kutokana na maoni hayo ya Henry. Jibu lake lilikua hivi, “Henry hajakutana na hasira za mashabiki 60,000 moja kwa moja kwasababu yeye kwanza anakaa kwenye viti bora vya ghahara ambapo hakuna mashabiki wenye hasira huko anapokaa. Hayo ni mawazo yake lakini hajakutana mara nyingi na kiwango cha hasira cha mashabiki”.
Wenger aliendelea,“Hayo ni mawazo yake na ni haki yake, Mashabiki wataendelea kuwa nyuma yetu na sina wasiwasi juu ya hilo.Siku zote kwenye soka tunafanya 98% na tunahitaji kutafuta hizo 2%.”

No comments:

Post a Comment