Wednesday, 18 March 2015

MAAJABU..MBUZI AZALIWA NA VICHWA VIWILI..JIONEE

DSC00655
Mbuzi mmoja katika Kijiji cha Kakanjuni Kenya amezaa mbuzi mwenye vichwa viwili vilivyoungana huku akiwa na midomo miwili, tukio hili limewashangazawengi walioshuhudia huku wengine wakihisi kwamba mbuzi huyo ni mkosi.

Tuesday, 17 March 2015

YULE MSIEMPENDA KAACHIWA HURU..SASA NGUMI ZOTE ULINGONI..

cheeeUnakumbuka ile skendo iliyompata bondia wa ngumi nchini Francis Cheka baada ya kumpiga na kumuumiza meneja wa baa yake akimtuhumu kusababisha hasara?

Thursday, 5 March 2015

MVUA YA MASAA MAWILI YALETA MAJANGA MKOANI SHINYANGA,,ZAIDI YA WATU 30 WAPOTEZA MAISHA

'Mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kiamkia leo imeuwa watu zaidi ya 50 na wengine zaidi ya 80 kujeruhiwa katika kijiji cha Mwakata kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mvua hiyo iliyonyesha majira ya saa 4 za usiku ilidumu kwa muda wa masaa mawili ikiambatana na upepo mkali na mawe yaliyopelekea watu hao kupoteza maisha na wengine kujeruhiwa na kuharibu mazao  pamoja na miti .

Kamanda wa Polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha alifika eneo la tukio akiwa sambamba na mkuu wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya ambao wametoa pole kwa wafiwa pamoja na mikakati ya serikali kuangalia utaratibu wa kusaidia kaya zilizobakia.
Hata hivyo bado idadi kamili ya athari kwa ujumla ukiacha vifo vya watu haijatolewa.

Mi naungana na waombolezaji kuwapa pole ndugu jamaa na marafiki walioondokewa  na ndugu zao katika janga hili.'
Vua kubwa iliyonyesha usiku wa kiamkia leo imeuwa watu zaidi ya 50 na wengine zaidi ya 80 kujeruhiwa katika kijiji cha Mwakata kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Tuesday, 3 March 2015

Wimbo wa Marehemu Kapteni Komba Wamliza Rais Kikwete,Ally hassan mwinyi.

Wimbo wa John Komba aliouimba katika msiba wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere mwaka 1999, jana uliibua majonzi na kusababisha viongozi mbalimbali, akiwamo Rais Jakaya Kikwete, kutoa machozi ulipoimbwa kumuaga mbunge huyo.Wimbo huo uliobadilishwa maneno yanayohusu Mwalimu Nyerere na kuingizwa yanayomtaja mbunge huyo wa Mbinga Magharibi, mbali na Rais Kikwete ulimliza pia Rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, Spika wa Bunge, Anne Makinda, Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, Katibu Mkuu mstaafu wa CCM, Yusuf Makamba na waombolezaji wengine.
Sehemu ya mashairi ya wimbo huo uliokwenda kwa jina la “Nani Yule” ulioimbwa na wanamuziki mbalimbali wa bendi nchini, na kuwatoa watu machozi iliimbwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye.
“Kapteni Komba familia yako umeiacha na nani, chama chako umekiacha na nani, nenda baba msalimie Mwalimu, mweleze hali ya Watanzania ilivyo hivi sasa, mweleze hali ya nchi yetu ilivyo hivi sasa hasa wakati huu, msalimie Mzee Kawawa Simba wa Vita”
Baadhi ya wanamuziki walioshiriki kuimba wimbo huo ni King Kiki, Mbunge wa Viti Maalumu, Martha Mlata, Jose Mara ambaye ni mwanamuziki wa bendi ya Mapacha Watatu na Luiza Mbutu wa African Stars.