HATIMAYE bilionea Moise Katumbi Chapwe, Rais wa klabu ya TP Mazembe ya DRC amekubali mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta ajiunge na KRC Genk ya Ligi Kuu ya Ubelgiji. Na Samatta anatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho kwa ajili ya safari ya Ubelgiji kwenda kuanza maisha mapya katika soka ya Ulaya. Samatta tayari amekwishasaini Mkataba wa awali na Genk wa miaka minne na sasa anakwenda kukamilisha taratibu. Samatta na Genk wanataka kukimbizana na muda ili kuwahi kabla ya dirisha dogo la usajili halijafungwa, angalau mapema Februari Mwanasoka huyo Bora Anayecheza Afrika aanze kucheza Ubelgiji.
Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo amesema kwamba Katumbi ameridhia Samatta aende klabu anayopenda.