]]
Presha juu: Pep Guardiola yupo hatarini kupoteza umoja katika vyumba vya kubadilishia nguo katika klabu ya Bayern Munich
PEP
Guardiola anapigana vita ya ndani kwa ndani katika klabu yake ya
Bayern Munich baada ya kazi yake kuingia dosari msimu huu katika
michuano ya UEFA, huku akihusishwa kuelekea ligi kuu soka nchini
England.
Mhispani
huyo alifika ujerumani mwanzoni mwa msimu huu na tayari ameshashinda
taji la Bundesliga, UEFA Super Cup na kombe la FIFA la klabu bingwa ya
Dunia.
Lakini
kocha huyo wa zamani wa Barcelona anapigana vita ya kukishawishi kikosi
chake kiendeleza mafanikio waliyoyapa siku za karibuni.
Licha
ya kushinda makombe matatu msimu huu, kipigo cha aibu walichokipata
Bayern kutoka kwa Real Madrid hatua ya nusu fainali ya UEFA kimeibua
maswali juu ya hatima yake ya baadaye.
Kuna mitazamo kuwa timu imeshuka kiwango chini ya Guardiola, na hii inahusishwa na kipigo kutoka kwa Carlo Ancelotti.
Mbaya
sana kuna kundi la wachezaji wanaanza kuunga mkono mitazamo hii , hivyo
Guardiola kuwa hatarini kupoteza umoja wa wanandinga wake.
Kuna
hisia miongoni mwa watu kuwa umoja mkubwa wa timu ilioachwa na Louis
van Gaal na Jupp Heynckes umeanza kupotea chini ya Guardiola.
Gwiji
wa soka wa Bayern Franz Beckenbauer wiki iliyopita alionesha kuumizwa
sana na kiwango cha timu hiyo kufuatia kipigo walichoambulia kutoka kwa
Real.
No comments:
Post a Comment