Kurugenzi ya mawasiliano Ikulu jijini Dar es salaam nchini Tanzania
imetoa tahadhari kwa wananchi juu ya kuwepo kwa baadhi ya watu ambao ni
matapeli na wanatumia vibaya jina la ikulu kwa kusema kwamba kuna nafasi
za ajira na wana uwezo wa kuwapatia ajira kwa kutoa fedha.
Tahadhari hiyo imetolewa jana jijini Dar es salaam na Mkurugenzi wa
mawasiliano Ikulu Bw. Salva Rweyemamu wakati alipokuwa akizungumza na
waandishi wa habari kufuatia kutokea kwa matukio kadhaa ya mfululizo ya
watu kutapeliwa kwa kutafutiwa kazi ikulu.
Aidha Salva amesema Rais Jakaya Kikwete anatarajiwa kufanya maamuzi ya
watuhumiwa wa kashfa ya Tegeta Escrow ambao walikuwa wakifanyiwa
uchunguzi kama alivyoahidi wakati wa mkutano wake na wazee wa mkoa wa
Dar es salaam tarehe 22 mwezi Disemba mwaka jana.
No comments:
Post a Comment