MWANZILISHI wa mashindano ya urembo ya
Miss Tanzania , Prashant Patel , amefungua
maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Dar es Salaam akiomba mshirika
wake, Hashim Ludenga , azuiliwe kuendelea
kuendesha mashindano hayo yanayotarajiwa
kufikia kilele chake Oktoba 11, mwaka huu.
Patel amewasilisha maombi hayo katika hati
ya dharura kupitia wakili wake, Benjamin
Mwakagamba , akidai Lundenga ana mpango
wa kuendesha mashindano hayo kwenye
Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam,
kinyume cha sheria na bila hata kumtaarifu.
Anaomba mahakama itoe zuio dhidi ya
Lundenga , la kuendesha mashindano hayo
hadi shauri lake la msingi aliloliwasilisha
litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi . Katika
kesi yake ya msingi, Patel anadai pamoja na
mambo mengine, utekelezaji wa makubaliano
ya Februari 20 , 2012 na malipo ya Sh milioni
19 ambayo hayajalipwa kwa mujibu wa
mkataba na faida nyinginezo ambazo
zimejitokeza hadi Septemba 23, mwaka huu.
Shauli hilo limepangwa kutajwa mbele ya
Hakimu Mkazi Mwandamizi Frank Moshi leo ,
na Lundenga ametakiwa kuwasilisha utetezi
wake ndani ya siku 21 , na akishindwa
kufanya hivyo , mahakama itaendelea kutoa
hukumu dhidi yake. Katika hati ya kiapo
inayounga mkono maombi yake , Patel anadai
kuwa yeye pamoja na Lundenga ndio
waanzilishi, waongozaji na waendeshaji wa
mashindano ya Miss Tanzania na wamekuwa
katika hali hiyo kwa miaka 20 sasa , tangu
mashindano hayo yaliyoporuhusiwa tena
mwaka 1994 . Kwa kipindi chote hicho,
wamekuwa wakisaini makubaliano ya namna
ya kuendesha mashindano hayo na mara ya
mwisho walisaini makubaliano Februari 20,
2012. Hata hivyo , Lundenga alikataa kusaini
makubaliano kwa mwaka 2013 na 2014 na
ameshindwa kumlipa fedha zake Sh milioni
19. Patel anadai badala yake Ludenga
ameshirikiana na wadhamini wengine
kuendesha mashindano hayo. Kwa mujibu wa
makubaliano , Lundenga pia alipaswa kulipa
pauni za Uingereza 30, 000 kama malipo ya
kibali kwa mwendeshaji wa shindano hilo
duniani, Miss World, deni ambalo limekuwa la
muda mrefu, hivyo kuchafua hadhi yake .
Patel anadai kuwa Ludenga alipelekewa
taarifa na wakili wake kulimaliza suala hili
bila kushirikisha hatua za kisheria , lakini
alikaidi na kukataa . Hivyo Patel anadai kuwa
hakuwa na njia nyingine zaidi ya kulipeleka
suala hilo mahakamani
Tuesday, 7 October 2014
MAHAKAMA HUENDA IKAZUIA KUFANYIKA KWA MISS TANZANIA 2014
Kumekucha : Maalim Seif Hamad Kujiuzulu Umakamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar...
Hali ya mambo visiwani Zanzibar siyo nzuri
hata kidogo, (wala si ya kufurahia) toka jana
jioni ilipotoka taarifa ya kufukuzwa kazi kwa
Mwanasheria Mkuu wa SUK Athuman Masoud.
Kumekuwa na vikao usiku kucha kwa viongozi
na wanachama wa CUF Zanzibar, na kuazimia
pamoja na mambo mengine kufanya tathimini
ya "KUJIUZULU" kwa makamo wa kwanza wa
rais wa serikali ya umoja wa kitaifa. Maalim
Seif.
Naam, mmoja wa vijana aliepewa kazi ya
kupima upepo ambaye ni mwanasheria wa
CUF, anaangalia swala hili kisheria
(ikumbukwe kuna makubaliano ya kisheria
katika kuongoza SUK).
Baadhi wamepewa angles tofauti na kutoa
majibu mapema iwezekanavyo.
Ili Mheshimiwa achukue uamuzi Mgumu
haraka leo.
Kama ikiwa ndio hivyo, kesho Media zote ni
kujiuzulu kwa Sharif na si kupokeaji wa katiba.
My take:
Kama karidhia yeye mwenyewe Mh.Maalim, na
iwe hivyo ila kama ni kupata attention ya
media tu siyo.
Viboko vyatembezwa makaburini Sengerema
Wajukuu wa marehemu Sabina Ngalu wa
Mwanza wamecharazwa viboko na watoto wa
marehemu baada ya kung’ang’ania kaburini
wakitaka wapewe fedha.
Chanzo cha wajukuu hao zaidi ya 10
kucharazwa bakora ni kung’ang’ania ndani ya
kaburi lililokua limeandaliwa kwa ajili ya
kuhifadhi mwili wa marehemu wakitaka
wapewe ng’ombe mmoja au sh.100,000 kama
zinavyotaka mila za kabila la kisukuma.
Gazeti la MTANZANIA ambalo lilikua shuhuda
katika eneo hilo lilisema kitendo hicho kilimkera
Padri Nicodemus Mayalla aliyekua akiendesha
ibada eneo hilo huku akiwataarifu polisi kuhusu
vurugu hizo hata hivyo kaka mkubwa wa
marehemu aliamua kuchukua fimbo na kuanza
kuwachapa.
Kitendo cha kuwachapa kiliamsha hasira zaidi
kwa wajukuu hao ambao nao walijibu kwa
kurusha michanga wakiwa ndani ya kaburi hadi
waombolezaji walipoamua kuchanga na
kuwapa fedha hizo ndipo walipotoka.
Hata hivyo Padri huyo aligoma kurejea eneo la
makaburi kuongoza ibada hadi hapo watoto
hao watakaporudisha fedha hizo na kuomba
radhi,jambo ambalo lilitekelezeka.
BARCELONA KUTIMULIWA LA LIGA IWAPO KATALUNYA ITAJITENGA HISPANIA
KLABU ya Barcelona haitaruhusiwa kucheza
La Liga ikiwa Katulonya itajitenga kutoka
Hispania, Mkuu wa ligi ya nchi hiyo, Javier
Tebas amesema hayo juu ya uwezekano wa
mgawanyiko wa taifa hilo mwezi ujao.
Tebas amefafanua kwamba sheria za
michezo za nchi hiyo zinaruhusu nchi moja
tu ambayo si sehemu ya Hispania - Andorra
- kushiriki ligi hiyo au mashindano mengine,
na FC Andorra tayari inacheza katika mfumo
wa za Hispania.
Huku La Liga tayari ikionekana kuwa na
timu mbili zinazochuana vikali kwenye vita
ya mataji (pamoja na Atletico Madrid
kushinda taji msimu uliopita kuzima utawala
wa Real na Barca kwa misimu tisa)
kuwapoteza vigogo hao wa Katalunya
litakuwa pigo kubwa kwa soka ya Hispania.
Vigogo wa Hispania, Barcelona moja kwa
moja watakuwa wamejiondoa La Liga ikiwa
Katalunya litakuwa taifa huru
"Ikiwa Katalunya litakuwa taifa huru, kwa
kuzingatia Sheria za Michezo Hispania,
kwamba Barcelona haitaruhusiwa kucheza,"
Tebas, rais wa LFP, amewaambia Waandishi
wa Habari mjini Barcelona.
"Yatahitajika mabadilika katika sheri a
zilizowekwa na Bunge la Hispania. Wazi,
iwapo itatokea litakuwa pigo kubwa katika
soka ya Hispania kuwap[oteza Barca.
"Sipati picha LFP bila Barca. Kwa namna
hiyo hiyo siwezi kupata picha Katalunya bila
Hispania, Siioni La Liga bila Barca. Pia ikiwa
itatokea hivyo, utaiitaje hiyo ligi: Ligi ya
Hispania au Ligi ya Iberia?'
Sababu ambazo zimeipa Andorra fursa ya
kucheza ligi ya Hispania, nchi ndogo
kwenye milima ya Pyrenees
inayozitenganisha Hispania na Ufaransa-
zinaweza kutumika pia kuzifanya klabu za
Katalunya ziendelee kushiriki.
Barcelona, ikiwa na nyota kama Lionel Messi
katika timu yao, watabaki kucheza Ligi ya
Katalunya
Xavi na Gerard Pique ni miongoni mwa
wachezaji wa Barca waliojitokeza
kuunga mkono kung a mkono kujitenga kwa
Katalunya. Serikali ya Katalunya itaamua
Oktoba 15 juu ya mustakabali wa nchi yao.