Tuesday, 7 October 2014

Viboko vyatembezwa makaburini Sengerema

Wajukuu wa marehemu Sabina Ngalu wa
Mwanza wamecharazwa viboko na watoto wa
marehemu baada ya kung’ang’ania kaburini
wakitaka wapewe fedha.
Chanzo cha wajukuu hao zaidi ya 10
kucharazwa bakora ni kung’ang’ania ndani ya
kaburi lililokua limeandaliwa kwa ajili ya
kuhifadhi mwili wa marehemu wakitaka
wapewe ng’ombe mmoja au sh.100,000 kama
zinavyotaka mila za kabila la kisukuma.
Gazeti la MTANZANIA ambalo lilikua shuhuda
katika eneo hilo lilisema kitendo hicho kilimkera
Padri Nicodemus Mayalla aliyekua akiendesha
ibada eneo hilo huku akiwataarifu polisi kuhusu
vurugu hizo hata hivyo kaka mkubwa wa
marehemu aliamua kuchukua fimbo na kuanza
kuwachapa.
Kitendo cha kuwachapa kiliamsha hasira zaidi
kwa wajukuu hao ambao nao walijibu kwa
kurusha michanga wakiwa ndani ya kaburi hadi
waombolezaji walipoamua kuchanga na
kuwapa fedha hizo ndipo walipotoka.
Hata hivyo Padri huyo aligoma kurejea eneo la
makaburi kuongoza ibada hadi hapo watoto
hao watakaporudisha fedha hizo na kuomba
radhi,jambo ambalo lilitekelezeka.

No comments:

Post a Comment