MWANZILISHI wa mashindano ya urembo ya
Miss Tanzania , Prashant Patel , amefungua
maombi katika Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu, Dar es Salaam akiomba mshirika
wake, Hashim Ludenga , azuiliwe kuendelea
kuendesha mashindano hayo yanayotarajiwa
kufikia kilele chake Oktoba 11, mwaka huu.
Patel amewasilisha maombi hayo katika hati
ya dharura kupitia wakili wake, Benjamin
Mwakagamba , akidai Lundenga ana mpango
wa kuendesha mashindano hayo kwenye
Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam,
kinyume cha sheria na bila hata kumtaarifu.
Anaomba mahakama itoe zuio dhidi ya
Lundenga , la kuendesha mashindano hayo
hadi shauri lake la msingi aliloliwasilisha
litakaposikilizwa na kutolewa uamuzi . Katika
kesi yake ya msingi, Patel anadai pamoja na
mambo mengine, utekelezaji wa makubaliano
ya Februari 20 , 2012 na malipo ya Sh milioni
19 ambayo hayajalipwa kwa mujibu wa
mkataba na faida nyinginezo ambazo
zimejitokeza hadi Septemba 23, mwaka huu.
Shauli hilo limepangwa kutajwa mbele ya
Hakimu Mkazi Mwandamizi Frank Moshi leo ,
na Lundenga ametakiwa kuwasilisha utetezi
wake ndani ya siku 21 , na akishindwa
kufanya hivyo , mahakama itaendelea kutoa
hukumu dhidi yake. Katika hati ya kiapo
inayounga mkono maombi yake , Patel anadai
kuwa yeye pamoja na Lundenga ndio
waanzilishi, waongozaji na waendeshaji wa
mashindano ya Miss Tanzania na wamekuwa
katika hali hiyo kwa miaka 20 sasa , tangu
mashindano hayo yaliyoporuhusiwa tena
mwaka 1994 . Kwa kipindi chote hicho,
wamekuwa wakisaini makubaliano ya namna
ya kuendesha mashindano hayo na mara ya
mwisho walisaini makubaliano Februari 20,
2012. Hata hivyo , Lundenga alikataa kusaini
makubaliano kwa mwaka 2013 na 2014 na
ameshindwa kumlipa fedha zake Sh milioni
19. Patel anadai badala yake Ludenga
ameshirikiana na wadhamini wengine
kuendesha mashindano hayo. Kwa mujibu wa
makubaliano , Lundenga pia alipaswa kulipa
pauni za Uingereza 30, 000 kama malipo ya
kibali kwa mwendeshaji wa shindano hilo
duniani, Miss World, deni ambalo limekuwa la
muda mrefu, hivyo kuchafua hadhi yake .
Patel anadai kuwa Ludenga alipelekewa
taarifa na wakili wake kulimaliza suala hili
bila kushirikisha hatua za kisheria , lakini
alikaidi na kukataa . Hivyo Patel anadai kuwa
hakuwa na njia nyingine zaidi ya kulipeleka
suala hilo mahakamani
Tuesday, 7 October 2014
MAHAKAMA HUENDA IKAZUIA KUFANYIKA KWA MISS TANZANIA 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment