BEKI mpya wa Manchester United, Marcos Rojo
anaweza kuichezea kwa mara ya kwanza klabu
yake hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England
dhidi ya Queens Park Rangers Uwanja wa Old
Trafford Septemba 14 baada ya kupatiwa hati ya
kufanya kazi.
Rojo alisafiri hadi Lisbon Alhamisi ili kukamilisha
taratibu za kupata hati hiyo ya kufanyia kazi
England.
Kufanikiwa kwa mchezaji huyo kupata hati hiyo
ya kufanyia kazi ni faraja kwa kocha Louis van
Gaal, ambaye kikosi chake mina tatizo la safu ya
ulinzi.
Uthibitisho: Marcos Rojo amepatiwa hati ya
kufanyia kazi maana yake sasa anaweza
kuichezea Manchester United kwa mara ya
kwanza dhidi ya QPR
Thursday, 4 September 2014
MARCOS ROJO APATIWA KIBALI CHA KUPIGA MZIGO MAN UNITED, VAN GAAL SASA ROHO KWATUUU
RONALDO AFUNGUA MTIMA WAKE; "MAN UNITED IPO MOYONI MWANGU, NATAMANI
MWANASOKA Bora wa Dunia, Cristiano Ronaldo
amesema kwamba Manchester United ni klabu
ambayo ipo moyoni make na anatamani siku
moja are jee kucheza tena.
Mchezaji huyo wa Real Madrid na Ureno
ameweka wazi "MaipendaI Manchester," na
kuongeza;
"Kila mmoja anajua hilo — nimesema hivyo mara
nyingi. Manchester ipo moyoni mwangu.
Nimeacha marafi wengi huko, mashabiki
wanavutia sana na ninatamani siku moja
ningerudi,".
Monday, 1 September 2014
KWA MZIKI HUU BADO MANCHESTER UNITED ITASHINDWA KUINUKA KWELI?
DIRISHA LA USAJILI LAFUNGWA; WALIOTOKA NA KUINGIA KLABU ZOTE ENGLAND HADI SEKUNDE YA MWISHO WAKO HAPA
![]() |
Mtu wa kazi; Radamel Falcao amehamia Manchester United kwa mkopo kutoka Monaco ya Ufaransa |
VAN GAAL AHAMIA KWENYE UKUTA, AMNASA BEKI BORA WA UHOLANZI KUTOKA AJAX
Unaweza kudhani Louis van Gaal amelala na anasajili washambuliaji tu, la! Wakati dirisha la usajili linakwenda ukingoni kufungwa, Manchester United imemnasa beki kisiki wa Ajax, Daley Blind.
WELBECK AENDA KUFANYIWA VIPIMO VYA AFYA ARSENAL....FALCAO ACHUKUA NAFASI YAKE OLD T.
KLABU ya Arsenal inapambaa dakika za
mwishoni kuelekea kufungwa dirisha la usajili
kuhakikisha inakamilisha uhamisho wa
mshambuliaji wa Manchester United, Danny
Welbeck kwa dau la Pauni Milioni 6.
Hiyo inafuatia The Gunners kumkosa
mshambuliaji wa Monaco, Radamel Falcao,
ambaye amehamia Manchester United leo.
Hivi sasa inaelezwa Welbeck anafanyiwa vipimo
vya afya Arsenal kukamilisha uhamisho huo.
CHICHARITO AFAULU VIPIMO VYA AFYA, RASMI NI MCHEZAJI WA REAL MADRID
MSHAMBULIAJI Javier Hernandez amekamilisha
uhamisho wake wa mkopo kwenda Real Madrid
pamoja na uwezekano wa kununuliwa moja kwa
moja kutoka Manchester United baadaye.
Real inamchukua mchezaji huyo baada ya
kufaulu vipimo vya afya leo mjini Madrid.
United inataka dau la Pauni Milioni 17 kumuuza
moja kwa moja mchezaji huyo, lakini kwa
mkataba wa sasa wa mkopo wa muda mrefu wa
msimu, Louis van Gaal anachukua Pauni Milioni
1.5.
United imethibitisha katika ukurasa wake wa
Twitter leo kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo
kwenda Real Madrid.