BEKI mpya wa Manchester United, Marcos Rojo
anaweza kuichezea kwa mara ya kwanza klabu
yake hiyo katika mchezo wa Ligi Kuu ya England
dhidi ya Queens Park Rangers Uwanja wa Old
Trafford Septemba 14 baada ya kupatiwa hati ya
kufanya kazi.
Rojo alisafiri hadi Lisbon Alhamisi ili kukamilisha
taratibu za kupata hati hiyo ya kufanyia kazi
England.
Kufanikiwa kwa mchezaji huyo kupata hati hiyo
ya kufanyia kazi ni faraja kwa kocha Louis van
Gaal, ambaye kikosi chake mina tatizo la safu ya
ulinzi.
Uthibitisho: Marcos Rojo amepatiwa hati ya
kufanyia kazi maana yake sasa anaweza
kuichezea Manchester United kwa mara ya
kwanza dhidi ya QPR
Thursday, 4 September 2014
MARCOS ROJO APATIWA KIBALI CHA KUPIGA MZIGO MAN UNITED, VAN GAAL SASA ROHO KWATUUU
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment