Monday, 1 September 2014

CHICHARITO AFAULU VIPIMO VYA AFYA, RASMI NI MCHEZAJI WA REAL MADRID

MSHAMBULIAJI Javier Hernandez amekamilisha
uhamisho wake wa mkopo kwenda Real Madrid
pamoja na uwezekano wa kununuliwa moja kwa
moja kutoka Manchester United baadaye.
Real inamchukua mchezaji huyo baada ya
kufaulu vipimo vya afya leo mjini Madrid.
United inataka dau la Pauni Milioni 17 kumuuza
moja kwa moja mchezaji huyo, lakini kwa
mkataba wa sasa wa mkopo wa muda mrefu wa
msimu, Louis van Gaal anachukua Pauni Milioni
1.5.
United imethibitisha katika ukurasa wake wa
Twitter leo kumtoa kwa mkopo mchezaji huyo
kwenda Real Madrid.

No comments:

Post a Comment