Hali ya hewani kuchafuka Bungeni hii
Duniani kote iko, ukiyaona leo Bongo sio mageni, kuna wakati utayaona
hayo hata kwenye Mijengo ya Mabunge ya wenzetu yaani.
Leo kubwa iliyokaa kwenye kurasa za mbele Magazetini, mitandaoni, ishu ya Wabunge wa upinzani Afrika Kusini kumkatisha Rais Zuma wakati
akihutubia Bungeni jana jioni FEBRUARY 12 na kuanzisha mzozo mkubwa
wakimtaka Rais huyo aeleze kuhusu tuhuma za Rushwa na Ufisadi
zinazomkabili.
“Tunamtaka Rais atujibu majibu mepesi; lini atarudisha pesa zetu“– alihoji Mbunge wa Upinzani, Julius Malema.
Spika wa Bunge Baleka Mbete alimtaka Malema
kutoka nje ambapo baada ya kuonekana akibisha kundi la askari walivamia
na kumtoa kwa nguvu ndani ya Jengo hilo pamoja na baadhi ya Wabunge,
ambapo baadaye Rais Zuma aliendelea na hotuba yake.
Mwezi Novemba 2014 Mbunge Mashabela aliwahi kutamka ndani ya Bunge hilo kuwa Rais Zuma ni mwizi hali ambayo ilichafua pia hali ya hewa kwenye Bunge hilo kwa kiasi kikubwa.
Hii ni video ya tukio la mwaka 2014
No comments:
Post a Comment