![couple2_rgb](http://i0.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/02/couple2_rgb.jpg?resize=503%2C335)
Katika hali ya kawaida imezoeleka kuwa
tendo la ndoa au mapenzi hufanywa zaidi na vijana kwa sababu miili yao
imechangamka na pia ina nguvu kuliko ya watu wazima na afya ya kuhimili
tendo hili lakini pia ule mvuto wa mapenzi nao huwa mkubwa miongoni mwa
vijana.
Kinyume na dhana za kawaida, Utafiti
mpya uliofanyika kwenye maeneo kadhaa ulimwenguni umeonyesha kuwa watu
wenye umri mkubwa wanaongoza kwa kufanya mapenzi mara nyingi kuliko watu
wenye umri mdogo ikiwemo vijana.
Ripoti zimeonyesha kuwa 31% ya wanawake
wenye umri kati ya 50 na 90 wanafanya mapenzi angalau mara mbili kwa
mwezi huku 54% ya wanaume wenye umri wa zaidi ya miaka 50 wanafanya
mapenzi angalau mara mbili kwa mwezi.
![Imegundulika kuwa wanawake ambao wana umri mkubwa hufurahishwa na tendo la ngono kirahisi kuliko wanaume .](http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/02/Couples-Therapy-Season-4-Episode-3-New-Couple-Controversy.jpg?resize=515%2C290)
Utafiti huu pia umeonyesha kuwa kiwango
cha kuridhishwa na tendo la ndoa huongezeka kwa wanawake kadri umri wao
unavyozidi kuongezeka huku ikiwa kinyume kwa wanaume ambao wanaonekana
kutoridhika na mapenzi kadri umri unavyozidi kwenda.
No comments:
Post a Comment