SIMBA, NA MBEYA CITY ZAINGIZA MILION 123
![kkls_e3cab.jpg](http://www.mjengwablog.com/images/kkls_e3cab.jpg)
Watazamaji 21,936 ndiyo waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo namba 32 ya VPL msimu wa 2013/2014 iliyomalizika kwa timu hizo kutoka sare ya mabao 2-2.
Viingilio katika mechi hiyo vilikuwa sh. 5,000, sh. 8,000, sh. 15,000 na sh. 20,000 huku kila klabu ikipata mgawo wa sh. 30,064,741.95 wakati Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa ni sh. 18,910,830.51. (P.T)
Mgawo
mwingine wa mapato hayo ni asilimia 15 ya uwanja sh. 15,287,156.92,
tiketi sh. 3,145,790, gharama za mechi sh. 9,172,294.15, Kamati ya Ligi
sh. 9,172,294.15, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh.
4,586,147.08 na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)
sh. 3,567,003.28.
Boniface Wambura Mgoyo
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
No comments:
Post a Comment