Thursday, 19 September 2013

Hii ndio video ya Criss (Mzungu) akiimba wimbo wa Diamond "Mbagala", na kuutafsiri kwa kizungu.EBU ITAZAMEEEEE

Kupitia you tube video ambayo ameiweka tangu August 2012, Criss (Mzungu) aaonekana akiimba wimbo wa Diamond unaojulikana kama Mbagala katika Acoustic version.
Criss amesema hii ni katika moja ya zoezi lake la kujifunza lugha, kwahiyo ameamua kuchagua wimbo huo wa kiswahili ambao anaupenda na kuutafsiri kwa lugha ya kizungu na pia akajifunza kuuimba..





Hiki ndicho alichokiandika Criss juu ya kuimba wimbo huu

As a language exercise, I picked a Swahili pop song that I like and attempted to transcribe the lyrics and learn to sing it. The Swahili lyrics are below as well as my attempted English translation. Mbagala is an impoverished district on the outskirts of the Tanzanian city Dar Es Salaam. I might have made some mistakes in the transcription or translation, so kama wewe ni Mswahili na unalo shauri lolote kuhusu maneno au tafsiri, niambie!


Mbagala by Diamond

Verse 1

Busara na upole
(Wisdom and kindness)
Na hekima niliyorithi kutoka kwa mama yangu, mama
(And knowledge which I inherited from my mother)
Vyote hukuvijali, ukaona silingani kabisa kuwa na wewe
(You didn't care about any of it, you saw that I'm too different to have you)
Kwa kuti na mkole, ukakata kabisa na shina la penzi langu na
(For the palm frond and tree, you completely cut the stem of my love)
Eti kisa mali, ukaona bora uniache mimi na uolewe
(Oh, because of money, you thought it good to leave me and get married)
Ile siku shehe namuona anachoma ubani
(That day I see the sheikh burning incense)
Unavishwa pete unakuwa mke wa fulani
(You are wearing a ring and are becoming someone's wife)
Niliumia sana, sana
(I was hurt badly)
Ile siku shehe namuona anachoma ubani
(That day I see the sheikh burning incense)
Unavishwa pete unakuwa mke wa fulani
(You are wearing a ring and are becoming someone's wife)
Niliumia sana, niliumia sana, sana
(I was hurt badly, I was hurt so badly)

Chorus

Tatizo kwetu Mbagala, hapa nyumba mbele jalala
(The trouble in Mbagala, at the house here in front of the dump)
Tatizo kwetu Mbagala, ukaona mapenzi siwezi
(The trouble in Mbagala, you saw I cannot love)

Verse 2

Ungejua jinsi gani
(If you knew how...)
Machozi lolia kwa uchungu wa penzi langu na
(The tears which were cried for the pain of my love)
Mwenzio jinsi gani, vile nimeumia moyoni
(Your friend how, the way my heart aches)
Hata kupendwa sitamani
(I don't even want to be loved)
Utamu wa mapenzi mwenzako umekula kwangu ma
(The sweetness of love, your friend, you have consumed mine)
Mwenzio sitamani, hata raha tena mi sioni
(Your friend, I don't desire it, I can't feel even comfort again)
Nasikia hivi sasa una mtoto anaitwa Mamu
(I hear that now you have a child named Mamu)
Vile akinuna mpaka tabasamu
(The way she frowns or smiles)
Mmefanana sana, sana
(You both look so similar)
Mi mwenzako tena mapenzi mi sina hamu
(Me, your friend, I have no hunger for love again)
Tena na mpango wa kuhama Dar Es Salaam
(And I plan to leave Dar Es Salaam)
Nataka niende mbali, niepuke vita na walimwengu
(I need to get far away, to escape the war and the people of this world)
Mi mwenzenu siwezi
(Me, your friend, I cannot)

No comments:

Post a Comment