Saturday, 21 September 2013

Drogba aitoa hofu Ivory cost

drogba e16d2
TIMU ya soka ya taifa ya Ivory Coast, imepata nguvu mpya baada ripoti kusema nahodha wake, Didier Drogba, hana matatizo ya kiafya na yupo fiti kuivaa Senegal katika mechi ya mchujo ya kufuzu fainali za Kombe la Dunia zitakazofanyika Brazil mwakani. (HM)

Straika huyo mwenye umri wa miaka 35, katikati ya wiki iliyopita alitolewa kwenye mechi ya kichapo cha mabao 6-1 wakati kikosi chake cha Galatasaray kilipomenyana na Real Madrid katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya. Alionekana kama amepata maumivu
.
Hali hiyo ililitia hofu taifa lake, lakini ripoti za hivi karibuni zimedai kwamba Drogba hakupata maumivu makali na kwamba atakuwa fiti kwa mchezo wa kwanza hatua ya mtoano utakaofanyika mwezi ujao. Klabu yake ilidai kwamba mchezaji huyo amepata maumivu kidogo ya bega, lakini si kiwango kikubwa na kwamba hadi wiki ijayo atakuwa amepona kabisa.
Kocha wa Ivory Coast, Sabri Lamouchi, alikiri kwamba muda wote alikuwa akisali asipangiwe Senegal, lakini dua zake hizo ziligonga mwamba.:

No comments:

Post a Comment