Mbio za usajili wa kiungo wa kati katika klabu ya Manchester United zilileta vituko na maneneo mengi sana katika dirisha la
Cesc
Fabregas alikuwa chaguo la kwanza lakini kadri muda ulivyokuwa ukienda
ndivyo ilivyoonekana wazi asingeweza kuondoka Barca. Kiungo wa Athletic
Bilbao Ander Herrera alikuwa kiungo mwingine aliyetakiwa kama ilivyokuwa
kwa Luka Modric. Na wakati Arsene
Wenger akivunja kibubu na kulipa kiasi cha £42.5million kwa ajili ya
Mezut Ozil katika siku ya mwisho ya usajili, David Moyes akarudi kwenye
klabu yake ya zamani na kumsajili mchezaji wa Everton Marouane Fellaini
kwa ada ya uhamisho wa £27.5m – usajili ambao umemfanya mchezaji wa
zamani wa United Teddy Sheringham kusema kwamba klabu yake ya zamani
imemsajili mtu asiye sahihi.
Mchezaji ambaye hatofautiani sana na kiungo wa Manchester City Yaya Toure. Na Moyes akiwa anajiandaa na derby yake ya kwanza leo hii, upande mwekundu wa jiji la Manchester unaweza ukawa umempata mtu sahihi waliyekuwa wakimhitaji kwenye kiungo ambaye anaongeza uimara wa safu ya kiungo kama ilivyo kwa Yaya Toure kwa City.
Ni kweli, Fellaini anaweza akawa hana kipaji cha Ozil au jicho la pasi nzuri kama Fabregas, lakini mbelgiji huyu ameongeza kitu kikubwa katika safu ya kiungo ya United, dhidi ya Bayer wachezaji kama Robin van Persie, Wayne Rooney, Antonio Valencia na Shinji Kagawa, walipata uhuru mkubwa wa kucheza wakiwa na ulinzi mzuri wa Fellaini na ndio maana waliweza kuleta madhara makubwa kwa wapinzani wao.
Kitu kama hicho ndicho Toure
anachokifanikisha kwa timu ya City - kuwafanya washambuliaji wacheze kwa
uhuru chini ya ulinzi wake.
Kama ilivyoonekana katika ya Crystal Palace
na Bayer Leverkusen - Moyes atakuwa akimtumia zaidi Fellaini katika
kiungo cha kuziua pembeni ya Micheal Carrick.
Kule City, Toure, amekuwa akitumika kwa namna
mbili kama kiungo wa juu na muda mwingine akicheza chini zaidi, kwa
sasa akiwa anashirikiana na kiungo aliyesajiliwa kwa £30million
Fernandinho.
SIFA ZAO ZA KIMWILI
UREFU | UZITO | |
---|---|---|
Yaya Toure | 189cm | 90kg |
Marouane Fellaini | 194cm | 95kg |
Kiukweli kabisa katika dunia ya soka hivi
sasa ni wachezaji wachache wanaweza kucheza anavyocheza kiungo wa Ivory
Coast, akitumia zaidi nguvu, akili katika kuitawala safu yote ya
kiungo.
Moyes atakuwa akiomba na kutumaini Fellaini,
kiungo mkabaji wa kwanza kusajiliwa na timu hiyo katika kipindi cha
miaka sita, ataweza kucheza kama anavyocheza Toure katika safu ya kiungo
ya United.
Akiwa Fellaini atacheza kama alivyocheza usiku wa Jumanne, basi vita ya safu ya kiungo baina yake na Toure
itachangia sana katika matokeo ya mwisho ya mchezo huo unaopigwa katika
dimba la City of Manchester Stadium jumapili ya leo.
TAKWIMU ZA FELLAINI VS YAYA TOURE MSIMU ULIOPITA
No comments:
Post a Comment