Friday, 27 September 2013

LIGI KUU TANZANIA BARA KUENDELEA WIKI END HII, YANGA KUFUTA MACHUNGU NA RUVU??

Print PDF
>>VINARA SIMBA JUMAPILI NA JKT RUVU
>>AZAM, COASTAL WAGENI MBEYA!!
RATIBA
Jumamosi Septemba 28
Yanga v Ruvu Shooting
Rhino Rangers v Kagera Sugar
Mbeya City v Coastal Union
Mgambo JKT v JKT Oljoro
Jumapili Septemba 29
Ashanti United v Mtibwa Sugar
JKT Ruvu v Simba
Tanzania Prisons v Azam FC
++++++++++++++++++++++
VPL_2013-14_LOGO-NEWMabingwa Watetezi wa VPL, LIGI KUU VODACOM, Yanga, wanarejea tena kwenye Ligi wakitoka kwenye kipigo cha 3-2 walichokipata Jumapili iliyopita toka kwa Azam FC na Jumamosi wapo Uwanja wa Taifa Jijini Dar es Salaam kuwakaribisha Ruvu Shooting.
Kichapo hicho cha Azam FC kimeifanya Yanga ishike Nafasi ya 9 kwenye Ligi ikiwa na Pointi 6 kwa Mechi 5 baada kushinda Mechi moja, Sare 3 na Kufungwa moja huku wapinzani wao wa Jumamosi, Ruvu Shooting, wakiwa Nafasi ya 4 na wana Pointi 9 kwa Mechi 5.
Vinara wa Ligi hii, Simba, wenye Pointi 11, wao watacheza Jumapili na Ruvu JKT ambao wako Nafasi ya Pili wakiwa na Pointi 9.
Timu za Azam FC na Coastal Union, ambazo pia zina Pointi 9 kama vile JKT Ruvu na Ruvu Shooting, zote zipo huko Mbeya ambapo Jumamosi Coastal Union wataivaa Mbeya City na Jumapili Tanzania Prisons wataikabili Azam FC.
VPL-MSIMAMO:
NA
TIMU
P
W
D
L
GD
GF
POINTI
1
Simba SC
5
3
2
0
9
13
11
2
JKT Ruvu
5
3
0
2
4
6
9
3
Azam FC
5
2
3
0
3
8
9
4
Ruvu Shooting
5
3
0
2
3
6
9
5
Coastal Union
5
2
3
0
3
5
9
6
Kagera Sugar
5
2
2
1
3
6
8
7
Mbeya City
5
1
4
0
1
6
7
8
Rhino Rangers
6
1
4
1
0
7
7
9
Yanga SC
5
1
3
1
3
10
6
10
Mtibwa Sugar
5
1
3
1
-1
4
6
11
JKT Oljoro
5
1
1
3
-2
3
4
12
Mgambo JKT
5
1
1
3
-8
2
4
13
Prisons FC
5
0
3
2
-6
2
3
14
Ashanti United
6
0
1
5
-11
2
1

No comments:

Post a Comment