Saturday, 9 November 2013

MANCHESTER UNITED V ARSENAL.OLD TRAFFORD KESHO,HIZI NDIZO TAKWIMU ZA TIMU HIZI


ARSENAL_TEAM-INDONESIAMAN_UNITED-DAVID_MOYES_BENCH
 Tayari Mechi 10 zimeshachezwa kwenye Ligi na Arsenal bado wanachanja mbuga wakiwa Tayari Mechi 10 zimeshachezwa kwenye Ligi na Arsenal bado wanachanja mbuga wakiwa hawajafungwa tangu wabamizwe 3-1 na Aston Villa kwenye Mechi ya kwanza ya Ligi Msimu huu.

Wikiendi iliyopita, Arsenal, wakiwa Nyumbani Emirates, ndio walipata Mechi ngumu kwao kwenye Ligi Msimu huu walipoifunga Liverpool 2-0 kwa Bao za Santi Cazorla na Aaron Ramsey ambae Msimu huu anang’ara sana.
Safari hii, Arsenal wanatinga Old Trafford Uwanja ambao hawajashinda tangu Mwaka 2006 na Miaka miwili iliyopita walitwangwa Bao 8-2 na Mabingwa wa England Manchester United.

USO kwa USO:
Man United v Arsenal Mechi 175
-Man United Ushindi 75
-Arsenal Ushindi 60
-Sare 40

Lakini safari hii, Man United ipo chini ya Meneja mpya David Moyes baada ya kustaafu kwa Sir Alex Ferguson aliedumu Old Trafford kwa Miaka 26 na chini ya Moyes Mabingwa hawa walianza Msimu kwa kusuasua na kupokea vichapo kwenye Ligi toka kwa Man City, Liverpool na West Brom lakini sasa hali yao imebadilika kwa kushinda Mechi 3 za Ligi kati ya 4 walizocheza mwisho.

ARSENAL UWANJANI OLD TRAFFORD TANGU 2006:
3 Novemba 2012: Man United 2-1 Arsenal (Ligi Kuu)
28 Agosti 2011: Man United 8-2 Arsenal (Ligi Kuu)
12 Machi 2011: Man United 2-0 Arsenal (FA Cup)
13 Desemba 2010: Man United 1-0 Arsenal (Ligi Kuu)
29 Agosti 2009: Man United 2-1 Arsenal (Ligi Kuu)
16 Mei 2009: Man United 0-0 Arsenal (Ligi Kuu)
29 Aprili 2009: Man United 1-0 Arsenal (UEFA Championz Ligi)
13 Aprili 2008: Man United 2-1 Arsenal (Ligi Kuu)
16 Februari 2008: Man United 4-0 Arsenal (FA Cup)


Mabadiliko hayo ya Man United yanatokana na kuibuka kwa Chipukizi Adnan Januzaj na kupanda chati kwa Wayne Rooney aliepachika Bao 7 na kutoa msaada kwenye Bao 3 katika Mechi zao za mwisho 10 za Mashindano yote.
Lakini Arsenal, wakisakata Soka safi la kitimu, wanafungua nafasi nyingi na hili linaonyeshwa kwenye takwimu zao ambapo Olivier Giroud ametengeneza nafasi 10 za kufunga na yeye na Ramsey na Mesut Ozil wamesaidia Magoli mara 4.
Kwenye Mechi hii, Arsenal wataimarika zaidi kwa kupona kwa Kiungo wao Mathieu Flamini na Winga Theo Walcott.

No comments:

Post a Comment