Friday, 1 November 2013

LIGI KUU UINGEREZA NI PATASHIKA JUMAMOSI HII EMIRATES, ARSENAL v LIVERPOOL!

>>WENGER ANAAMINI GIROUD NI KIBOKO KUPITA ‘SAS’, SUAREZ & STURRIDGE!
>>CHELSEA KUFUNGUA JUMAMOSI ST JAMES PARK NA NEWCASTLE!!
>>MABINGWA MAN UNITED NDANI YA CRAVEN COTTAGE NA FULHAM!!
>>MAN CITY: KIPA JOE HART BENCHI…. PANTILIMON NAMBA 1!!
RATIBA
Jumamosi Novemba 2
[Saa za Bongo]
1545 Newcastle v Chelsea

1800 Fulham v Man Utd

1800 Hull v Sunderland

1800 Man City v Norwich


1800 Stoke v Southampton

1800 West Brom v Crystal Palace

1800 West Ham v Aston Villa

2030 Arsenal v Liverpool

 Ligi Kuu England, Jumamosi inaingia Mechi zake za 10 kwa Msimu huu na Mechi 8 zitachezwa Jumamosi na mbili Jumapili lakini Mechi ya Jumamosi Uwanjani Emirates kati ya Arsenal na Liverpool ndio BIGI MECHI.
Lakini habari kubwa huko England ni uamuzi wa Meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini kumbwaga Kipa wa England Joe Hart na kuamua Kipa Nambari mbili Costel Pantilimon, anaetoka Romania, kucheza Mechi yao ya Jumamosi na Norwich City Uwanjani Etihad.
Joe Hart amekuwa akilaumiwa kwa makosa makubwa na hasa Wikiendi iliyopita wakati yeye na Sentahafu wake Matija Nastasić walipojichanganya na kumruhusu Fernando Torres kuifungia Chelsea Bao la Pili na la ushindi Uwanjani Stamford Bridge Chelsea walipoifunga Man City 2-1.
Nae Arsene Wenger, akikabiliwa na BIGI MECHI ndani ya Emirates kati ya Timu yake Arsenal na Liverpool, ametoa matumaini makubwa alipodai Sentafowadi wake Olivier Giroud ni Sentafowadi wa uhakika kupita na Luis Suarez na mwenzake Daniel Sturridge ambao hivi sasa kwenye Ligi Kuu England wamebatizwa jina ‘SAS’ likimaanisha kile Kikosi maalum cha Jeshi Uingereza cha Makomandoo ‘Special Air Services’.
Wenger aliwania kumnunua Luis Suarez kabla Dirisha la Uhamisho kufungwa Septemba 2.
Suarez, ambae alichelewa kuanza kucheza Mechi za Ligi Msimu huu akimalizia Kifungo chake cha Mechi 10 alichopewa Mwezi Aprili kwa kumng’ata meno Beki wa Chelsea Branislav Ivanovic, Msimu huu kwenye Ligi amefunga Bao 6 katika Mechi 5.
Matumaini makubwa ya Arsenal kwa Magoli ni Olivier Giroud ambae hadi sasa amecheka na nyavu mara 8 na Wenger amesisitiza hilo aliposema: “Ikiwa Klabu zilitaka kumnunua Suarez ni sababu ya kucheza vizuri lakini kwa sasa mie mkazo wangu ni Wachezaji wa Arsenal. Naamini tangu Msimu huu uanze Giroud ni Straika wa kipekee na atatimiza hilo kwenye Mechi hii. Yeye na Suarez wana staili tofauti lakini Giroud ni Sentafowadi wa ukweli wakati Suarez ni mpiga chenga!”
Mechi za Ligi Wikiendi hii zitaanza Jumamosi kwa Mechi ya mapema kabisa huko St James Park wakati Newcastle watakapocheza na Chelsea.
Mabingwa Man United wapo Ugenini Craven Cottage kucheza na Fulham.

No comments:

Post a Comment