![SAMATTA+SUPER+CUP+DRC](http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/11/SAMATTA+SUPER+CUP+DRC.jpg)
![mbwana+samata](http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/11/mbwana+samata-1024x685.jpg)
Samatta na Ulimwengu walianza katika kikosi cha Mazembe pamoja na Tressor Mputu Mabi, lakini hawakuweza kuwanusuru mabingwa mara nne Afrika na kipigo hicho.
Sfaxien timu pekee iliyoshinda Kombe la Shirikisho mara mbili tangu kutambulishwa kwa mfumo mpya mwaka 2004, yenye makao yake makuu katika mji uliozungukwa na bahari ya Mediterranean, Sfax itahitaji sare katika mchezo wa marudiano au kufungwa kwa tofauti isiyozidi bao 1-0, mjini Lubumbashi ili kujinyakulia taji.
Bingwa wa Kombe hilo atazawadiwa kitita cha dola za Kimarekani, 625 000, wakati mshindi wa pili atapata dola 432 000.
Mshindi pia atakutana na mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, Al Ahly ya Misri kuwania taji la Super Cup mechi itakayochezwa nchini Misri Februari 2014.
![Ulimwengu+Thomas](http://millardayo.com/wp-content/uploads/2013/11/Ulimwengu+Thomas.jpg)
No comments:
Post a Comment